Necta yatangaza matokeo kidato cha pili, nne 2019
- Imetangaza matokeo ya upimaji kitaifa darasa la nne, kidato cha pili na nne ya mitihani iliyofanyika Novemba 2019.
- Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019 yanaonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kidogo kwa asilimia 1.4 kutoka ule wa mwaka 2018.
Dar es Salaam. Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, ametangaza matokeo ya upimaji kitaifa darasa la nne, kidato cha pili na nne ya mitihani iliyofanyika Novemba 2019.
Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019 yanaonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kidogo kwa asilimia 1.4 kutoka ule wa mwaka 2018. Licha ya ufaulu huo kuongezeka, bado takriban nusu ama asilimia 48.6 ya watahiniwa wote wa mwaka 2019 wamepata daraja la nne.
Necta imeeleza leo kuwa katika mtihani huo wanafunzi 340,914 wamefaulu mtihani kati ya wanafunzi 422,722 waliofanya mtihani huo Oktoba mwaka jana ikiwa ni sawa na asilimia 80.65 ya watahiniwa wote.
Hii ni sawa na kusema kuwa wanafunzi 81 kati ya 100 waliofanya mtihani huo wamefaulu.
Ufaulu huo, kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, ni sawa ongezeko la asilimia 1.38 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2018. Mwaka juzi asilimia 79.27 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo.
Soma zaidi:
- Necta yatangaza matokeo kidato cha pili, nne 2019
- Matokeo kidato cha nne haya hapa
- Shule 10 bora zilizotikisa matokeo kidato cha nne 2019
Takwimu za matokeo ya upimaji kidato cha pili zinaonyesha kuwa jumla ya wanafunzi 514,251 sawa na asilimia 90.04 kati ya 571,137 wenye matokeo ya upimaji wamepata ujuzi na maarifa kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu. Kati yao, wasichana ni 270,750 na wavulana ni 243,501.
Dk Msonde aliyekuwa akitangaza matokeo hayo leo (Januari 9, 2020) amesema pia matokeo ya upimaji kitaifa darasa la nne (SFNA) nayo yametoka.
Matokeo hayo yanapatikana katika tovuti ya Necta. Ili kuyapata matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019 bonyeza hapa. Na ya kidato cha pili bonyeza hapa.
TANGAZO: