Umuhimu wa tuzo,utambulisho kwenye biashara yako

January 28, 2020 10:10 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Kupata tuzo ni zaidi ya kutambulika kwani itakufungulia milango ya wawekezaji
  • Pia ni moja kati ya vitu vitakavyokupatia ari ya kufanya kazi
  • Hata ivyo wadau wamesema ni vema kuangalia usije ukawa “Awardpreneur”

Dar es Salaam. Wakati ukianza biashara yako, unakuwa na hamu ya kuiona ikizidi kusoga mbele kuwafikia watu wengi zaidi.

Hata hivyo, endapo biashara yako itaanzishwa na watu hawatoona umuhimu au uwepo wake, huenda ukakata tamaa na kuona kuwa hawaendani na mapokeo ya bidhaa yako sokoni au huduma, siyo nzuri.

Wadau mbalimbali wakiwemo wafanya biashara wamesema, wapo vijana ambao wana ona aibu kuomba kushiriki kwenye vinyang’anyiro mbalimbali vinavyokuja mbele yao licha ya kuwa na sifa zote.

Makala hii inakusogeza karibu wewe kama mfanyabishara kuanza kuangazia fursa hii ambayo ipo wazi kwaajili yako,Kwanini ushiriki?

Tuzo na Utambulisho zinasaidia kukuza soko la biashara yako

Mkurugenzi wa kampuni ya kidijitali inayojihusisha na ufundi pamoja na ujenzi ya Toolboksi, Julius Mbungo amesema wafanya biashara wengi wanaweza wasilione hili lakini, tuzo na utambulisho zinasaidia kwenye kukuza masoko ya kampuni yako kimataifa.

“Unapopokea hiyo tuzo, watu wengi wanapata kuifahamu bidhaa na huduma yako lakini zaidi, hata waliokuwa hawaifahamu kwa undani, wanapata fursa hiyo,” amesema Mbungo.

Wafanya biashara wengi wanaweza wasilione hili lakini, tuzo na utambulisho zinasaidia kwenye kukuza masoko ya kampuni yako kimataifa. Picha| Julius Mbungo.

Tuzo zinafungua milango ya kupata wawekezaji

Endapo kampuni yako inahitaji wawekezaji, ni heri ukaanza kulichangankia jambo hilo na kuliweka katika mipango yako .

Mbungo amesema, kushiriki kwenye tuzo hizi kutakusaidia kutambulika na hivyo kukupatia urahisi kupata wawekezaji kwani kupitia tuzo hizo, wanaweza wakawa wamekufahamu.

Zaidi, Mbungo amesema tuzo zitakusababishia “Spotlight” (Hali ya kutazamwa) na vyombo vya habari hasa kama huduma yako inagusa jamii.

Inaongeza ari ya kufanya kazi kwa kampuni au mtu binafsi

Kupokea tuzo ni kama kujulikana kwa kitu ambacho unakufanya. Hilo litakusaidia kuona kuwa kazi yako inaumuhimu na watu wanaifurahia.

“Hakuna kitu kizuri kama kufahamu kuwa wateja wako wanaipenda bidhaa yako. Utajuaje? Wao ndio watakao kupigia kura kuipata hiyo tuzo,” amesema Jessica Mshama ambaye licha ya kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya J Sisters, ni mshindi wa Tuzo ya Malkia Ajaye Tanzania na Mjasiriamali wa mwaka kutoka Tuzo za Starqt za Afrika kusini.

Upatikanaji wa kipato cha ziada.

Baadhi ya tuzo huja na zawadi ambayo inaweza ikawa ni pesa taslimu na hata safari ya kwenda mataifa mengine.

Kupitia pesa ambayo utaipata utakaposhinda, unaweza kufanya maendeleo makubwa kwenye kampuni yako ikiwemo kuboresha mazingira ya wafanyakazi na hata kununua vitu kadha wa kadha.

Inaongeza thamani yakampuni yako

Wakili kutoka kampuni Sheria Kiganjani ambayo ni kampuni ya kidijitali inayojihusisha na masuala ya sheria, Jumanne Nabiry amesema “kupitia tuzo hiyo, wadau mbalimbali wataithamini kampuni au huduma yako.”

Nabiry amesema Kampuni ya Sheria Kiganjani imejinyakulia tuzo ziadi ya tano hadi sasa ikiwa na miaka chini ya miwili na manufaa ya tuzo hizo yameonekana.


zinazohusiana


Hata hivyo, wadau hawa wameonya kwa wafanyabiashara, endapo hawatakuwa na msimamo, ni rahisi kupoteza mwelekeo wao na kuwa watu wanaotafuta tuzo pekee.

Mbungo amesema ni muhimu kufanya kazi kwa nguvu zote kwani kupitia kazi zako, tuzo zitakutafuta wewe na hautakuwa na shida ya kuzitafuta.

“Usipoangalia unaweza kupoteza muelekeo na kuishia kuwa awardpreneur (mjasiriamali anayetafuta tuzo,” amekazia Mbungo.

Naye Jessica  ameshauri wafanya biashara kufuatilia tuzo ambazo zinaridhisha kwani sikuhizi kila mtu anaanzisha tuzo zake.

“Siyo kila tuzo wewe unaenda tu. weka malengo yako juu, tafuta tuzo ambazo zina maana kwenye kazi zako a ambazo hata ukiwaambia watu watasema kweli hapa umefanya kazi” amesema Jessica akitolea mfano wa utambulisho kwenye jarida la Forbes na mengineyo yenye tija.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW