Ahueni kwa wanunuzi, bei ya maharage ikishuka Dar

February 28, 2020 3:13 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Gunia la kilo 100 la maharage limeshuka hadi Sh280,000 kutoka Sh300,000 ya ijumaa Februari 21, 2020. 
  • Bei hiyo ya maharage ni ya juu zaidi kuliko mazao yote ya chakula yanayouzwa leo katika masoko mbalimbali nchini. 
  • Bei ya chini kabisa ya maharage imeshuhudiwa katika masoko ya Halmashauri ya Musoma mkoani Mara ambapo gunia la kilo 100 limeuzwa kwa Sh100,000.

Dar es Salaam. Wanunuzi wa maharage katika jiji la Dar es Salaam leo watapata ahueni baada ya bei ya gunia la kilo 100 la zao hilo kushuka kwa Sh20,000 ikilinganishwa na bei iliyorekodiwa ijumaa Februari 21, 2020. 

Mazao makuu ya chakula hujumuisha mchele, maharage, viazi mviringo, mahindi, mtama, uwele, ulezi na ngano.

Takwimu za bei za mazao makuu ya chakula zinazotumika katika maeneo mbalimbali nchini zilizotolewa leo (Februari 28, 2020) na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaeleza kuwa gunia la kilo 100 katika soko la Kinondoni jijini humo linauzwa kwa Sh280,000 kutoka Sh300,000 ya wiki iliyopita. 

Hiyo ni sawa kusema bei ya maharage ya gunia la kilo 100 imeshuka kwa asilimia 6.6 ndani ya wiki moja. 

Hiyo itawapa ahueni wanunuzi na kuwaletea maumivu wafanyabiashara wa zao hilo ambao walitegemea bei ingeendelea kupanda ili kupata faida maradufu. 

Licha ya kuwa bei ya maharage imeshuka, bado bei hiyo inayotumika leo ndiyo bei ya juu zaidi kuliko mazao yote ya chakula yanayouzwa leo katika masoko mbalimbali nchini Tanzania.


Zinazohusiana


Bei ya chini kabisa ya maharage imeshuhudiwa katika masoko ya Halmashauri ya Musoma mkoani Mara ambapo gunia la kilo 100 limeuzwa kwa Sh100,000.

Takwimu hizo pia zinaonyesha kuwa viazi mviringo ndiyo vinauzwa kwa bei ya chini kabisa kuliko mazao yote makuu ya chakula yaliyopo sokoni leo. 

Bei hiyo imeshuhudiwa katika soko la Mwanjelwa mkoani Mbeya ambapo gunia la kilo 100 linauzwa kwa Sh46,000, wakati bei ya juu ya zao hilo ikiwa ni Sh120,000 katika mkoa wa Lindi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV