Utalii wa kimataifa kushuka kwa asilimia 30

March 27, 2020 3:39 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Shirika la Utalii Duniani (WTO) linasema idadi ya watalii wa kimataifa itashuka kwa kati ya asilimia 20 na 30 kutokana na kusambaa kwa ugonjwa wa virusi vya corona. 

Shirika hilo linasema mamilioni ya watu waliojariwa katika sekta ya utalii watakuwa katika hatari ya kupoteza kazi zao kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo. 

Taarifa ya shirika hilo lenye makao yake mjini Madrid Uhispania iliyolewa jana (Machi 26, 2020) inaeleza kuwa kupungua kwa idadi ya watalii kutasababisha hasara zaidi ya dola za Marekani bilioni 300 (Sh693.7 trilioni) katika utalii wa kimataifa. 

Duru za kimataifa zinaeleza kuwa virusi hivyo vya corona vinaonekana kusababisha athari kubwa zaidi ikilinganishwa na majanga yaliyopita kwani mwaka 2009 dunia ilipokumbwa na mzozo wa kifedha utalii ulishuka kwa asilimia 4 na mwaka 2003 kulipokuwa na virusi vya SARS vilivyowauwa watu 774 kote duniani, utalii ulishuka kwa asilimia 0.4. 

Shirika hilo mwanzoni mwa mwaka lilikuwa limekadiria kukuwa kwa utalii duniani kwa kati ya asilimia tatu na nne ila lililazimika kufanya mahesabu yake upya mwezi huu wa Machi baada ya kushuhudia kusambaa kwa virusi vya corona.

Enable Notifications OK No thanks