Wagonjwa watano wa Corona wapona Tanzania, wagonjwa wakifika 24

April 7, 2020 11:39 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Wizara ya Afya imesema wagonjwa wengine wawili wamepona leo na kufanya idadi ya waliopona kufikia watu watano mpaka sasa. 
  • Watu 72 wamewekwa karantini kwa uchunguzi zaidi.
  • Serikali yawataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote za kujikinga.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa wagonjwa wengine wawili waliokuwa na maambukizi ya ugonjwa virusi vya Corona wamepona na kufanya idadi ya waliopona kufikia watu watano mpaka sasa. 

Amesema wagonjwa waliopona ugonjwa huo wa COVID-19 unaosambaa kwa kasi duniani, mmoja anatoka jijini Dar es Salaam na mwingine Arusha. 

“Hivyo sasa Mkoa wa Arusha hauna mtu mwenye maambukizi ya COVID19,” amesema Ummy katika ukurasa wake wa Twitter leo (Aprili 7, 2020).

Licha ya Tanzania kuwa na visa 24 vya wagonjwa wa Corona, Waziri huyo amesema leo Aprili hakuna kisa kipya cha mgonjwa wa ugonjwa huo kilichothibitishwa leo.  

Kati ya wagonjwa hao waliothibitishwa kuwa na Corona, mmoja kati yao ambaye alifariki dunia wiki iliyopita kikiwa ni kifo cha kwanza Tanzania.


Zinazohusiana


Katika ukurasa huo, Ummy ameeleza kuwa watu 72 wamewekwa karantini  kwa ajili kuchunguzwa huku wengine 366 wanaendelea kufuatilia kwa karibu. 

Hata hivyo, wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya kunawa mikono mara kwa mara, kutokugusa pua, mdomo au macho, kutumia tishu wakati wa kukohoa au kupiga chafya na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima. 

/
No matches found for this filter
30 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV