Serikali kushusha tozo maendeleo ya ufundi (SDL)
June 11, 2020 2:23 pm ·
Mwandishi
- Zimeshushwa kutoka asilimia 4.5 hadi asilimia 4 ili kuwapunguzia waajiri mzigo na gharama za uendeshaji.
- Kwa muda mrefu waajiri wamekuwa wakilalamikia uwepo wa kiwango kikubwa cha tozo hizo ambazo huathiri pia mapato yao.
Dar es Salaam. Serikali imependekeza kushusha kiwango cha tozo kwa ajili ya maendeleo ya ufundi stadi (Skills Development Levy) kutoka asilimia 4.5 hadi asilimia 4 ili kuwapunguzia waajiri mzigo na gharama za uendeshaji.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesema hatua hiyo inatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh42.07 bilioni.
“Lengo la marekebisho haya ni kuwapunguzia waajiri mzigo na gharama za uendeshaji wa shughuli zao na kutimiza azma ya kupunguza tozo hizi hatua kwa hatua bila kuathiri mapato kwa kiasi kikubwa,” amesema Dk Mpango.
Kwa muda mrefu waajiri wamekuwa wakilalamikia uwepo wa kiwango kikubwa cha tozo hizo ambazo huathiri pia mapato yao.
Latest
1 day ago
·
Fatuma Hussein
Viwango vya kubadilisha fedha Tanzania Machi 9, 2026
4 days ago
·
Lucy Samson
ATCL kuwarudisha Watanzania waliokwama Dubai
5 days ago
·
Fatuma Hussein
Viwango vya kubadilisha fedha Tanzania Machi 4, 2026
6 days ago
·
Fatuma Hussein
Bei ya maharage yaendelea kuwa kichomi Dar es Salaam