Facebook yaibuka na “Messenger” ya watoto
- Programu hiyo ni mahususi kwa ajili ya watoto wa miaka sita hadi 12.
- Mzazi anaweza kuhariri maudhui anayoyaona mtoto wake katika app.
- “Messenger for kids” haina matangazo na taarifa za mtoto wako hazitolewi kwa watoa matangazo.
Dar es Salaam. Kampuni inayosimamia mtandao wa kijamii wa FaceBook (www.facebook.com) imezindua programu tumishi (App) ya simu ya mawasiliano mahususi kwa ajili ya watoto wanaoishi barani Afrika.
App hiyo ya Messenger Kids umezinduliwa ili kuwawezesha watoto kuwasiliana na rafiki pamoja na familia pale wanapokuwa mbali nao.
“Messenger Kids imetengenezwa kwa ajili ya watoto lakini inaratibiwa na mzazi. Watoto wanaweza kuanzisha mawasiliano ya moja kwa moja na watapata vitu vingine vya kucheza navyo wakiwa kwenye mawasiliano hayo.
Vitu hivyo ni pamoja na barakoa, emoji na kucheza na sauti ili kuweka uhai kwenye mawasiliano yao,” imesomeka taarifa ya Faceboook iliyotolewa Juni 10, 2020.
Pia, Facebook imesema app hiyo itawawezesha wazazi kufuatilia mienendo ya kimawasiliano ya watoto wao pale wanapofanya maongezi ya video, sauti na hata ujumbe mfupi wa maneno.
Messenger for kids imeambatana na vitu kama barakoa, emoji na kucheza na sauti ili kuweka uhai kwenye mawasiliano ya watoto. Picha| Forbes.
Messenger Kids inayopatikana katika duka la programu la I store na Google Play Store
Facebook imeshirikiana na washauri wa vijana pamoja na wadau wengine kwa miaka mingi hivyo imezingatia usalama wa watoto kuhakikisha wanatengeneza bidhaa hiyo yenye kuratibiwa na wazazi huku ikiwasaidia watoto kuwasiliana kwa uangalifu mtandaoni.
Mkurugenzi wa Sera za Umma Afrika, Kojo Boakye amesema anafahamu kuwa wazazi wengi wanageukia teknolojia kuliko hapo awali ili kuwasaidia watoto wao kuwasiliana mtandaoni.
Kupitia faragha, usalama na usimamizi wa mzazi kwenye kitovu cha programu tumishi hiyo, Messeger Kids inatoa sehemu salama inayoratibiwa na mzazi kufanya hivyo,” amesema Boakye.
Zinazohusiana
- Facebook yaibuka na app nyingine kuwaunganisha watu mtandaoni
- Zawadi ya Mark Zukerberg: Facebook kuwakutanisha makapela mtandaoni
- Facebook yafanya maboresho utafutaji wa bidhaa mtandaoni
Kupitia programu hiyo, mzazi anaweza kufuatilia watu ambao mtoto wake anawasiliana nao, historia ya mawasiliano ya ujumbe, mawasiliano yaliyoshtakiwa na yaliyozuiliwa yakiwemo yale ambayo mtoto anahusika nayo, yawe maongezi ya video, ujumbe wa maandishi na kiwango cha mawasiliano kwa mwezi.
“Utaona mawasiliano ambayo mwanao ameyazuia na yale aliyoyaruhusu. Pia kama mtoto wako ameripoti ujumbe wowote,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Facebook.
Zaidi, kupitia programu hiyo, mzazi anaweza kufuta picha ambazo anaona hazimfai mtoto wake.
Facebook hiyo mahususi kwa watoto haina matangazo na hivyo kuwa sehemu salama kwa mtoto.
Latest
