Utapigwa: Hakuna mabilioni ya msaada wa corona yanatolewa na akaunti ya Facebook

July 4, 2020 4:40 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ujumbe huo unaosema watu wachague  herufi ya kwanza ya jina ili mtu ajue atapata msaada wa pesa kiasi gani  umetumika sehemu nyingi ulimwenguni.

Dar es Salaam. Kumekuwa  taarifa inayozagaa kwenye mtandao wa Facebook  kuwa kuna hela zinazotolewa kwa ajili ya kujikimu wakati huu wa janga la corona lakini taarifa hiyo siyo ya kweli na kwa lugha ya vijana wa sasa ni famba.

Taarifa hizo ambazo zimekuwa zikipatikana kupitia akaunti za Facebook ambazo zinatumia picha au majina ya watu maarufu duniani huambatana na maelezo ya jinsi ya kupata hela hizo.

Mathalani hapa Tanzania akaunti ya Facebook inayojulikana kwa jina la Dewiy Oll Shop ilitumia picha ya mcheza sinema Dwayne Johnson maarufu The Rock ikieleza kwa Kiingereza hivi:

“For all countries …!!! Hello congratulations for today for those  of you who are lucky and this is official (NOT FRAUD) we are publishing it to help people because the corona virus outbreak has prevented many people from working.Choose the first letter of your name and your gift matches your name.

(Kwa mataifa yote….!!! Habari hongera kwa wote wenye bahati leo. Huu sio utapeli tumechapisha kwa ajili ya kuwasaidia watu wakati wa mlipuko wa janga hili la Corona kwa sababu imezuia watu wengi kufanya kazi.Chagua herufi ya kwanza ya jina lako ili kujua zawadi inayolingana nayo)

Sehemu ya picha inayo sambamba kwenye mtandao wa Facebook PichaI Mtandao

Tumevumbua ukweli

Nukta Fakti imebaini kuwa akaunti yenye jina la Dewiy_Oll Shop inatumia  picha ya muigizaji wa filamu wa Marekani Dwayne Johnson kwa nia ovu kwa kuwa akaunti halisi ya muigizaji huyo Dwayne The Rock Johnson haielezi taarifa yoyote ya kugawa fedha za msaada kwa waathirika wa corona tofauti na inavyoelezwa.

Mashaka mengine kuhusu taarifa ya akaunti hiyo ya Facebook ya  Dewiy _Oll shop ina ujumbe sawasawa na  akaunti feki ya Mwanamfalme wa Dubai (Hamdan bin Mohammed Al Maktoum) inayodai kutoa pesa za corona kama ilivyo kwa akaunti hiyo. Akaunti sahihi ya Mwanamfalame huyo wa Hamdan bin Mohammed bin Rashid Al Maktoum wa Dubai ni Hamdan Bin Mohammed Bin Rashid Al Maktoum | Fazza na haina maelezo wala  taarifa yoyote kuhusu utoaji wa hela katika kipindi hiki cha corona.


Zinazohusiana:


Jambo jingine maandishi hayo ya Kiingereza yana mapungufu ya kisarufi yakiwemo matumizi yasiyo sahihi ya alama. Ukitazama kitita cha unaodaiwa msaada herufi A utabaini kuwa imewekwa nukta baada ya tatu kwenye kiwango kinachomaanisha milioni. Taasisi makini haiwezi kuacha makosa madogo madogo kama haya yatokee hasa kwa mradi mkubwa wa mabilioni kama huo unaodaiwa kutoa msaada kwa watu.

Kumbuka kuwa hakuna fedha za bure bure. Iwapo kuna msaada wa fedha unaohusiana na corona huwa kuna akaunti halali za taasisi zinazofahamika ambazo hueleza.

Endelea kujikita na ugonjwa wa virusi vya corona kwa kufuata masharti yanayotolewa na wataalamu wa afya ikiwemo kuvaa barakoa maeneo yenye mikusanyiko mikubwa na kuna mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji tiririka.

Enable Notifications OK No thanks