Tahadhari: Mashine za kukaushia mikono haziui virusi vya Corona

July 13, 2020 6:09 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema mashine hizo siyo njia sahihi ya kuua virusi vya COVID-19.
  • Kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka mara kwa mara na kutumia vitakasa mikono inaweza kukusaidia kujikinga na ugonjwa huo. 

Dar es Salaam. Huenda wewe ni miongoni mwa watu ambao wanatumia mashine za kukaushia mikono hasa ukiwa katika vyoo au maeneo ya umma na umekuwa ukiamini kuwa mashine hizo zinaweza kuua virusi vya Corona. 

Fahamu wazi kuwa mashine hizo hazina uwezo wa kuua virusi hivyo aina ya COVID-19 na unachokiamini hakina ukweli wowote. 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema mashine hizo siyo njia sahihi ya kuua virusi vya COVID-19.

Limewataka watu kuendelea kuchukua tahadhari ya kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka mara kwa mara na kutumia vitakasa mikono (sanitizers). 

“Baada ya mikono yako kuwa safi, unaweza kuikausha kwa kutumia karasi laini au kukausha kwa mashine,” imeeleza WHO na kubainisha kuwa mashine za kukaushia mikono zitumie baada ya mtu kunawa mikono. 


Zinazohusiana


Kutokana na mashine kutumiwa na watu wengi kwenye maeneo ya umma zinaweza kuwa sehemu za kusambaza COVID-19 hasa kama zitaguswa.

Unakumbushwa usiguse mashine hiyo wakati wa kuitumia ili kujikinga na maradhi ya ugonjwa huo. 

Corona bado ipo, tuendelee kuchukua tahadhari.

Enable Notifications OK No thanks