“Youtube DataViewer” itakavyokusaidia kubaini video feki mtandaoni

July 21, 2020 6:11 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni zana ya kidijitali inayotumika kuthibitisha video ya mtandaoni  kama ni ya kweli au uongo
  • Zana hiyo inaweza kutumiwa na mtu yoyote ili kujiweka salama dhidi ya upotoshaji.

Dar es Salaam. Licha ya kuwa video zinatengenezwa dunia kuwa sehemu muhimu ya kusambaza ujumbe kwa njia mbalimbali ikiwemo muziki, lakini baadhi ya video hizo hutumika kupotosha umma.

Katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona, baadhi ya watu wamekuwa wakitengeneza video ili kuzusha na kuwapotosha watu ili kujinufaisha.

Leo ningependa  tujifunze kuhusu zana za kidijitali ya “Youtube DataViewer” itakayokusadia kuthibitisha  video kama ni ya ukweli au uongo.

YouTube Data Viewer ni zana ya kidijitali inayopatikana kwa njia ya tovuti pekee na hutumiwa kwa ajili ya kuthitisha taarifa za mtandaoni.

Zana hiyo iliyotengenezwa na shirika la Amnesty International na inamilikiwa na taasisi ya Citizen Evidence Lab hutumiwa kwa ajili ya kuthibitisha taarifa kuhusu video hasa muda ambao video hiyo iliwekwa mtandaoni sambamba na  malezo  na picha za msingi kuhusu video hiyo.

Jinsi ya kuitumia

Kuitumia ni rahisi  unachotakiwa kufanya ni kutafuta neno “Youtube DataViewer” kwenye kitafutio cha Google na itakupa majibu kuhusu ulichokitafuta.

Baada ya kutafuta, Google itakuletea majibu kadhaa utatakiwa kufungua jibu la kwanza ambalo litakupeleka moja kwa moja Youtube DataViewer ili uweze kuitumia na kuithibitisha video husika.


Zinazohusiana:


Baada ya hapo, mtumiaji atatakiwa kuweka kiunganishi  (Link)  cha video ambacho nilazima kiwe kinatokana na  Youtube  ambapo ataweza kupata majibu ya aina tatu kichwa cha habari cha video hiyo, tarehe, mwezi na mwaka ambao video hiyo ilipopakiwa mtandaoni.

Ukiingiza kiunganisha hicho itakupa taarifa zote za video ikiwemo kama iliwahi kuchapishwa sehemu yoyote.

Enable Notifications OK No thanks