Unavyoweza kukabiliana na vipele vinavyotokana na kunyoa ndevu

October 16, 2020 12:00 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kutumia maji ya baridi punde unapoanza kuvihisi vipele hivyo usoni kwako
  • Paka mafuta maalumu kwenye kidevu baada ya kunyoa ndevu.

Dar es Salaam. Unadhifu wa devu zako hutegemea mambo mbalimbali ikiwemo namna unavyozitunza na kuzinyoa.

Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wanapata vipele baada ya kunyoa ndevu nyumbani, zipo dondoo muhimu zinazoweza kukusaidia kutatua changamoto hiyo ukaendelea kuwa na muonekano mzuri.

Je, unawezaje kukabiliana na vipele hivyo pale vinapotokea?

Kwa mujibu wa tovuti ya masuala ya maisha ya The Knot, hatua ya kwanza kukabiliana na vipele mara tu vinavyopoanza kujitokeza.

Mara nyingi vipele hivyo vinasababishwa na majeraha madogo madogo ambayo yanaachwa baada ya kunyoa.  

Kwa kuanza, nawa uso wako pamoja na kidevu kwa maji ya baridi na kisha pakaa mafuta yanayozuia ngozi kukauka (moisturerizer).

Pia, kwenye kabati au meza yako, usikose losheni maalum ya kupaka baada ya kunyoa. 

Kwa kufahamu jinsi ya kunyoa na usipate vipele, tazama video hii:

Enable Notifications OK No thanks