Internews, Nukta Africa waanza kuwanoa wanahabari kwa takwimu

November 9, 2020 9:09 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Mafunzo hayo yanayofanyika kwa njia ya mtandao yamezinduliwa leo na yatafanyika hadi Novemba 13, 2020. 
  • Waandishi wa habari 20 kutoka vyombo vya habari mbalimbali nchini Tanzania wanashiriki mafunzo hayo.
  • Mafunzo haya yanatolewa ili kuwajengea uwezo zaidi wa kuripoti habari za takwimu kwa usahihi.

Dar es Salaam. Kampuni ya teknolojia na habari Nukta Africa kwa kushirikiana na shirika lisilo kuwa la kiserikali la Internews wamezindua rasmi mafunzo maalum ya siku tano ili kuwajengea uwezo wanahabari wa Tanzania kuandika kwa usahihi habari za takwimu zenye mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii.

Mafunzo hayo yanayofanyika kwa njia ya mtandao yanafanyika kati ya Novemba 9 na 13, 2020 yanajumuisha waandishi wa habari 20 kutoka vyombo vya habari vya redio, televisheni, magazeti na vyombo vya mtandaoni (online media).

Mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Afrika, Nuzulack Dausen aliyekua akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo amesema mafunzo hayo yana umuhimu kutokana na mabadiliko ya teknolojia na ushindani unaotokea katika sekta ya habari nchini.

“Jamii siku hizi zinafanya maamuzi kwa kutumia takwimu lakini je, kama waandishi tumeisaidia jamii kupata takwimu hizo? Ni wakati sasa wa kujifunza ili tuandike habari zilizo na tija kwa Watanzania,” amesema Dausen.

Mafunzo hayo yatasaidia kuongeza idadi ya wanahabari wa Tanzania waliobobea katika uandishi wa habari za takwimu ambao unasaidia siyo tu kufanya maamuzi lakini kujenga misingi ya uwajibikaji na uwazi kwenye jamii. 

Afisa Mradi wa Boresha Habari kutoka Internews Tanzania,  Victoria Rowan amesema lengo kuu la mafunzo haya ni kuwawezesha Watanzania kupata habari sahihi za takwimu kutoka kwa wanahabari makini.

“Kwa muda sasa tumekuwa tukishirikiana na Nukta Africa katika kutoa mafunzo kwa ajili ya uandishi wa takwimu. Lengo letu ni kuwafikia waandishi wa habari wengi zaidi ili kuunufaisha umma wa Watanzania,” amesema Rowan.


Soma zaidi


Mafunzo hayo ambayo yalianza kutolewa mwaka 2018 kati ya Nukta Africa na Internews yamewanufaisha wanahabari 20 akiwemo Halili Letea kutoka gazeti la Mwananchi. 

Letea ambaye ni mnufaika wa mafunzo haya mwaka 2018/2019 amewataka wanahabari wanaoshiriki mafunzo ya wiki hii kuwasikiliza kwa makini wakufunzi na kuyatendea kazi watakayojifunza.

“Unachotakiwa kufanya ni kujifunza na kisha kuandika habari hizo kwa vitendo,” amesema Letea ambaye ni mshindi wa jumla wa tuzo za umahiri katika uandishi wa habari (EJAT) kwa mwaka 2019 zinazotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). 

Baada ya mafunzo hayo, wanahabari saba watakaowasilisha mawazo bora ya habari, watapata ruzuku kuwawezesha kuandika habari za takwimu zinazogusa maisha ya watu kwenye maeneo yao. 

Mwanahabari kutoka redio SAUT FM jijini Mwanza, Fadhili Mbalwa amesema mafunzo haya yatamuongezea mwanga katika kufanya kazi zake hasa zinazohusisha takwimu.

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV