Serikali yaeleza sababu kupungua usafirishaji mizigo uwanja wa ndege Mwanza

December 1, 2020 12:42 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Sababu mojawapo ni athari za janga la Corona baada ya baadhi ya nchi kusitisha usafiri wa ndege. 
  • Yakarabati sehemu ya kupakulia na kupakilia mizigo. 

Mwanza. Licha ya kutatua changamoto ya upakuaji wa mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwanza, kumeripotiwa upungufu wa shehena ya mizigo ikiwemo minofu ya samaki iliyokuwa ikisafirishwa kwenda barani Ulaya katika miezi miwili iliyopita kutokana na athari za janga la Corona. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk Leonard Chamuriho akizungumza hivi karibuni jijini Mwanza amesema ugonjwa wa Corona kwenye baadhi ya nchi za Ulaya umeathiri biashara na safari za ndege.

Amesema kwa muda sasa ndege nyingi hazijatua katika uwanja huo na  sababu nyingine ni kuwa nchi ambazo wateja huagiza minofu ya samaki wamesitisha kutoa oda kutokana na ugonjwa wa corona.

Dk Chamuriho amesema kwa sasa ni wateja wachache wanaoagiza mizigo hiyo na husafirishwa kwa kutumia ndege za abiria  kupitia viwanja vya Kilimanjaro (KIA) na Julius Nyerere (JNIA). 

“Maboresho ya mfumo wa ubebaji wa mizigo katika uwanja huo ni sehemu ya kujiweka tayari kukabiliana na soko la wateja baada ya kurejea tena kwa biashara baina ya Mwanza na mataifa ya Ulaya,” amesema Dk Chamuriho.


Zinazohusiana: 


Serikali imetumia zaidi ya Sh300 milioni  kutatua changamoto ya ubebaji wa mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa kutengeneza mfumo rahisi wa uchukuzi ambapo shehena ya mizigo itatelezeshwa kwenye reli maalum kabla ya kupakiwa kwenye ndege au wakati wa kupakuliwa.

Mfumo huo umekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia uwanja huo kusafirisha minofu  ya samaki kwenda barani Ulaya.

Meneja wa Uwanja wa ndege huo, Paschal Kalumbete aliyekua akizungumza hivi karibuni amesema mfumo utapunguza muda wa kupakia na kushusha mizigo na hivyo kulinda usalama wa mizigo hiyo ambayo haihitaji mitikisiko.

“Kabla ya hapo wafanyabiashara walitumia muda wa saa 1:30 kushusha na kupakia tani saba za mizigo kwenye ndege,  suala ambalo linalolalamikiwa si wafanyabiashara  tu hata watendaji  wa ndege,” amesema Kalumbete na kuongeza

“Kama mamlaka ya viwanja vya ndege tukaamua kuja na suruhisho kwa kupata mkandarasi aliyebuni mfumo huu ambao sasa shehana ya tani Saba itashushwa  au kupakiwa kwa daki 25 hadi 30.”

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV