Mitandao ya kijamii yamdhibiti Trump, Bunge la Marekani likithibitisha ushindi wa Biden

January 7, 2021 10:19 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Twitter yamzuia kuchapisha chochote kwa saa 12 ikitishia kuiuzia jumla akaunti hiyo iwepo ikiendelea kuvunja sera zake.
  • Facebook yamfungia kwa 24 kutokana na machapisho yake yaliyochea maandamano Washington D.C.

Dar es Salaam. Kampuni ya teknolojia ya Twitter imeendelea kukunjua makucha yake kwa Rais wa Marekani Donald Trump baada ya kuizua akaunti yake kwa Saa 12 kutochapisha na kumuamuru kufuta twiti tatu alizokuwa amezichapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao huo.

Uamuzi huo wa Twitter umekuja saa chache baada ya wafuasi wa Trump kufanya maandamano na kuvamia jengo la shughuli mbalimbali za bunge la nchi hiyo lijulikanalo kama Capitol Hill jijini Washington,D.C na kufanya vurugu.

“Kutokana na matukio ya vurugu zinazoendelea Washington, D.C tumeamuru kuondolewa kwa twiti tatu zilizokuwa zimechapishwa hapo awali na @realDonaldTrump kutokana na kujirudia kwa uvunjaji wa sera za uadilifu,” Twitter imesema kupitia ukurasa ambao hutoa taarifa mbalimbali wa @TwitterSafety.

Kutokana na uamuzi huo wa kuondoa twiti hizo, Twitter imesema ukurasa wa Trump utazuiwa kwa saa 12 na iwapo hatazitoa twiti hizo basi utaendelea kuzuiwa.

“Uvunjaji wa taratibu na kanuni zikiwemo sera za uadilifu na kuthibiti vurugu utakaofanywa hapo baadaye utasababisha kusimamishwa moja kwa moja kwa akaunti ya @realDonaldTrump,” kampuni hiyo imeeleza.

Mapema Jumatano Desemba 6, 2020 Trump alihamasisha wafuasi wake kuandamana ili kulipinga Bunge la Uwakilishi (Congress) la nchi hiyo kuthibitisha ushindi wa Rais mteule Joe Biden na makamu wake wa rais Kamala Harris.


Soma zaidi:


Kwa nyakati tofauti Trump amekuwa akidai kuwa ameshinda urais huku akituhumu kuwa kura zake ziliibwa. Madai hayo yametupiliwa mbali na mamlaka za kusimamia uchaguzi nchini humo.

Kutokana na kukithiri kwa tabia ya Trump ya kuchapisha madai ya kuibiwa kura, Twitter imekuwa ikiziwekea maelezo madogo (labels) twiti zenye utata kutoka kwa kiongozi huyo kuwa anayosema hayajathibitishwa.

Hata hivyo, mapema Alhamis 7 Januari 2021, bunge hilo lilimthibitisha Biden na Harris kuwa rais na makamu wa rais ajaye baada ya kuridhia kura za wajumbe 306, wengi zaidi ya 270 wanaohitajika. 

Viongozi hao wanatarajia kutwaa madaraka Januari 20, 2020.

Mbali na Twitter, Shirika la habari la Uingereza la Guardian limeeleza kuwa kampuni ya Facebook nayo imezuia Trump kuchapisha chochote katika mitandao yake ya Facebook na Instagram, aumuzi ambao umeeleza kuwa ni mgumu kufanywa kwa kiongozi wa taifa hilo tajiri ulimwenguni. 

Facebook imemzuia Trump kuchapisha kwa saa 24. 

Enable Notifications OK No thanks