Nje, ndani: Simu mpya ya Samsung ikiingia sokoni

January 21, 2021 7:41 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni simu ya Samsung Galaxy S21 ambayo itaingia soko Januari 29 mwaka huu.
  • Simu hii imeambatana na maboresho kidogo ikilinganishwa na S20 ya mwaka jana.
  • Tofauti na simu nyingine, hii itakua na mfuniko wa plastiki upande wa nyuma.
  • Kamera, uwezo wa uhifadhi vitu na nguvu ya betri ni sawa na S20.

Dar es Salaam. Ushindani kati ya Samsung na simu zingine unazidi kupamba moto kila kukicha huku ikiacha wadau wa teknolojia ya simu janja njia panda ya simu gani itawafaa kwa matumizi yao.

Kwa wateja wa simu za iPhone zinazotengenezwa na kampuni ya Apple ya nchini Marekani, walimaliza mwaka 2020 wakiwa na iPhone12 ambayo inauzwa kwa Sh2.55 milioni katika duka la mtandaoni la Apple.

Kwa sasa, ni zamu ya wadau wa simu za Samsung ambao kuanzia Januari 29, 2020 wajiandae kutoboa mifuko yao kwa Samsung Galaxy S21 ikiwa ni takriban mwaka mmoja tangu simu ya Samsung Galaxy S20 iingie sokoni Februari 11, 2020.

Kufuatia tangazo la kuionyesha simu hiyo rasmi lililotolewa na Samsung Januari 14 mwaka huu, haya ndiyo tunayoyafahamu kuhusiana na simu hiyo ijayo.

Kamera “bado nipo nipo”

Kwa kuwa ni simu mpya, tulitegemea itakuja na kamera iliyo na “megapixel” (MP) kubwa zaidi ya toleo la S20 lakini Samsung wameamua kuendelea kuwa na kamera ile ile japo imefanyiwa maboresho ambayo huenda yakawavutia zaidi wadau wa mitando ya kijamii ikiwemo Instagram.

S21 inaambatana na kamera yenye ukubwa wa MP 64 kwa kamera ya kupiga picha za mbali (telephoto), MP 12 kwa kamera ya upana (wide) na upana zaidi (ultrawide). 

Mfumo wa “super steady” ambao unamwezesha mtu kurekodi video isiyo na mitikisiko umeendelea kutumika.

Kamera ya mbele imebaki kuwa na MP 10 sawa na S20 jambo ambalo huenda likafanya wapenda picha wasiojali upya wa simu kuendelea kubaki na simu zao za zamani yaani S20.

Jambo lililofanywa na Samsung ni sawa na ilichofanya Apple katika simu yake ya iPhone12 ambayo kamera yake haitofautiani uwezo wa MP na iphone 11.

Kwa wapenzi wa kurekodi video, simu hii itawafaa kwani inatumia teknolojia ya “8K” ambayo ndiyo teknolojia ya juu zaidi katika kurekodi video bora katika simu janja.

Vitu vingine ambavyo havijabadilika katika simu hii ni pamoja na uwezo wa betri ambao umebaki kwenye 4000 mAh inayokadiriwa kuwasha simu kwa siku nzima bila kuchaji kulingana na matumizi ya mtu.

Simu hii itakuja na rangi nne ambazo ni “phantom” nyeupe, kijivu, pinki na zambarau (violet). Picha| Buro247.

Muonekano mpya

Samsung imetoa simu zilizotengenezwa na kioo mbele na nyuma tangu toleo la S6 hadi S20 lakini kwa toleo hili jipya, Samsung imeamua kurudisha plastiki katika sehemu ya nyuma kama yalivyokuwa matoleo ya awali likiwemo S5.

Kwa sasa S21 itakuja na kioo mbele, aluminiumu pembeni na sehemu ya kamera huku sehemu nyingine iliyobaki, ikiwa ni platiki.

Hatua hiyo huenda ikawa ni faraja kwa baadhi ya wadau wa Samsung ambao hawakufurahia kupasuka kwa sehemu ya nyuma ya simu pale simu inapodondoka. 

Hata hivyo, huenda waliofurahia simu iliyo na kio mbele na nyuma wakaaangushwa na mabadiliko hayo.

Simu hiyo inakadiriwa kuuzwa kuanzia Sh2.36 milioni katika duka la mtandaoni la Amazon huku ikipatiikana kwa manunuzi ya kabla (preorder) katika maduka ya samsung.


Soma zaidi:


Mengineyo

S21 imeongezeka uzito wa gramu sita kutoka gramu 163 ikilinganishwa na S20 huku ukubwa wake pia ukiongezeka kwa kufikia sentimita za mraba 94.1 ongezeko kidogo ikilinganishwa na simu ya mwaka 2020.

Pia simu hii inakuja na kizazi kipya cha mfumo endeshi wa Android 11 na mtumiaji wa S20 ataendelea kutumia simu hii ambayo ina uwezo wa kutumika hata ndani ya maji ya kina cha mita 1.5 kwa dakika 30.

Simu hii itakuja na rangi nne ambazo ni “phantom” nyeupe, kijivu, pinki na zambarau (violet) huku ikiambatana na matoleo dada ya S21 plus na S21 Ultra ambazo ni stori ya siku ingine.

Kazi kwako kutoboa mfuko ili kujipatia simu hiyo mwaka 2021. 

Enable Notifications OK No thanks