Hutaweza kutumia WhatsApp kwenye simu hizi ifikapo Januari mosi 2021
- Ni pamoja na baadhi ya simu za iPhone na Samsung.
- Simu hizo ni zile zilizotolewa kabla ya mwaka 2010.
- Baadhi ya watumiaji wa simu watatakiwa kusasisha simu zao.
Dar es Salaam. Msemo wa mwaka mpya na mambo mapya, huenda ukawakumba baadhi ya watumiaji wa simu ulimwenguni ambao maboresho ya mtandao wa WhatsApp yatawafanya kuukosa mtandao huo na hivyo kuwalazimu wanunue zingine.
WhatsApp ambao ni mtandao wa mawasiliano unaotumia intaneti kutuma meseji, ujumbe wa sauti na video, ni kati ya mitandao ya kijamii maarufu huku ukiwa na watumiaji zaidi ya miloni 100 wanaofurahia mawasiliano yanayovuka mipaka ya kimataifa kwa teknolojia ya simu na kompyuta.
Hata hivyo, mtandao huo unaomilikiwa na Facebook unatarajia kufanya maboresho ambayo yataanza kufanya kazi ifikapo Januari 1 mwakani ambayo yatasababisha mtandao huo usipatikane kwa baadhi ya simu zikiwemo za iPhone na Samsung.
Watumiaji wa simu za iPhone 4 na Samsung Galaxy S2 wanalazimikakununua simu mpya endapowatahitaji kutumia mtandao wa WhatsApp. Picha| YouTube.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Independent la Uingereza, simu zote aina ya iPhone 4 na Samsung Galaxy S2 hazitoweza kuutumia mtandao huo.
Siku nyingine ni zile zinazotumia mfumo endeshi wa ndroid zilizotolewa kabla ya mwaka 2010 zikiwemo HTC Desire, LG Optimus Black na Motorola Droid Razr.
Aidha, kwa baadhi ya simu pia bado zinahitaji kusasisha (update) mifumo endeshi yake kufikia IOS9 kwa simu za iPhone (zikiwemo Apple iPhone 4S, iPhone 5, iPhone 5S, iPhone 6 na iPhone 6S) na Android zifikie kiwango cha 4.0.3.
Soma zaidi:
- Teknolojia zilizotikisa Tanzania miaka 10 iliyopita
- Simu zachangia kushuka kwa redio majumbani Tanzania
- Umuhimu wa matangazo ya kidijitali kwa wafanyabiashara
Simu zingine ni pamoja na Samsung Galaxy S3, HTC Sensation, HTC Thunderbolt, LG Lucid, Motorola Droid 4 na Sony Xperia Pro.
Pia, kwa mwaka 2021, WhatsApp itatoa sera na sheria mpya za faragha ambazo utatakiwa kuzikubali ili kuendelea kutumia mtandao huo.
Zoezi hilo litafanyika mwanzoni mwa mwaka ujao na watakaoshindwa kukubaliana na sera hizo, watapoteza mazungumzo (chati) zao na uwezo wa kutumia mtandao huo ifikapo Februari 8, 2021.