Lupin, Bridgerton: Tamthilia zinazobamba mjini “Netflix”

January 22, 2021 10:20 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

  • Ni Tamthilia ambazo huenda umezisikia kwa watu mbalimbali.
  • Ni pamoja na filamu za “Lupin” na “Bridgerton” ambazo visa vyake huenda vikakuongezea ukaribu na simu yako.
  • Mafunzo ya familia, visasi na burudani ni kati ya vitu unavyotakiwa kujiandaa kuvipata endapo una miaka zaidi ya 16.

Dar es Salaam. Kwa wadau wa tamthilia za kwenye televisheni almaarufu kwa kimombo kama “Series” huenda programu tumishi ya Netflix inayoonyesha filamu hizo na zingine ikawa ni mahala pao kupatia burudani hiyo.

Kwa muda sasa, Netflix imekuwa ikibandika bandua filamu zinazokonga nyoyo za wengi ambao kiu ya kusubiria msimu (season) ujao huwa ni kubwa baada ya msimu mmoja kuisha. 

Kama wewe unatumia App ya Netflix na haufahamu filamu za kuangalia, huenda filamu hizi zikakufanya uzidi kuwa karibu na simu yako hasa App ya Netflix.

Tamthilia ya Lupin

Kwa wengi urithi kutoka kwa baba ni mali na vitu vingine vya kushikika lakini kwa Assane Diop, urithi alioachiwa na baba yake ni maarifa.

Kitabu anachopewa Diop kujisomea, kinageuka kuwa mkombozi wa maisha yake ya mbele kwa kuwa mbali na utanashati wake, ni mwizi anayestahili tuzo ya juu kuwahi kuwepo.

Diop, ambaye baba yake anajinyonga akiwa gerezani baada ya kusingiziwa kuiba mkufu wenye thamani kubwa na bosi wake, anaanza safari ya kuchimbua ukweli juu ya mkufu huo.

Diopp anaamua kuchimba ukweli nyuma ya upotevu wa mkufu huo ambao ni sababu ya kifo cha baba yake. Picha|Den of Geek.

Kijana huyo  ambaye baba yake alimuachia kitabu cha mwizi mtanashati “Arsene Lupin” anaishi maudhui ya kitabu hicho huku akitegua kila mtego unaopangwa kumkamata.

Hata hivyo, siyo yeye tu anayesoma kitabu hicho na huenda siku siyo nyingi atapata mtu wa kupambana naye.

Fuatilia tamthilia hii ujionee njiapanda ya familia ilivyo na nafasi kubwa katika uovu wa mtu.

Filamu hii ina sehemu tano zilizo na hadi dakika 52 hivyo huenda ukamaliza msimu mzima wa filamu hii ndani ya saa nne tu.


Soma zaidi:


Tamthilia ya Bridgerton

Inahitaji watu wawili kupendana, wawili kuitwa wapenzi na wawili kuoana. Lakini  kwa filamu ya Bridgerton, inahitaji mwanaume mmoja kupiga goti kupata ridhaa ya kumuoa binti ambaye mamia wanamtazama kama simba mwenye njaa atazamavyo swala anayepita mbele yake.

Ni msimu wa kutafuta wenzi ndani ya jiji la London na kwa falme hii inayosimamiwa na malkia Charlotte ni kawaida kumtambua mwana mwali mrembo kuliko wote. Na kwa muktadha huo, binti huyo ndiye swala miongoni mwa simba.

Asubuhi inayosubiriwa na wengi inawadia na kila mama anamuandaa bintiye ili atambulike kama mrembo wa msimu. Kuficha ukubwa wa tumbo, kuvalia nguo za kuvutia macho ni sehemu ya familia nyingi ikiwemo familia ya Bridgeeton na binti yao Daphne Bridgerton. 

Kama ilivyotarajiwa, Daphne mwenye muondoko wa twiga, tabasamu la tausi na ngozi mfano wa sufi, ndiye anayemulikwa na mwangaza wa malkia Charlotte. 

Simon ambaye aliapa mbele ya kitanda cha mauti cha baba yake kuwa hawezi kuoa, anabaki njiapanda baada ya moyo wake kudodndoka kwa binti Daphne. Picha| Netflix.

Bahati mbaya ni kuwa, kaka yake anageuka kikwazo kwa kuwafukuza wanaume wote wanaopendezwa na mrembo wa msimu. Hata hivyo, nguvu yake haifui dafu kwa Simon Basset ambaye ni Mkuu wa jimbo la Hastings ambaye bila kujua, anajikuta moyo umemdondokea binti Bridgerton.

Wahenga walisema kuwa mshumaa uwakao zaidi ndivyo huisha haraka. Kwa filamu hii, huenda masiha ya mshumaa yakalingana na ya binti Daphne ambaye kipeperushi cha mbea wa msimu, Lady Whistledown hakisiti kumtaja kila kukicha.

Visa vya kukata na shoka, umbea wa ufalme kutoka kwa Lady Whistledown na wivu wa kufisha kutoka kwa fanani wa filamu hii utakuacha ukitafuta saa moja ya kuangalia filamu hii iliyo na sehemu nane.

Huenda ukahitaji kujinoa zaidi kwani msimu wa pili wa filamu hii nao umetangazwa kuwa njiani.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV