TCRA yatangaza kanuni kudhibiti vifurushi vya simu Tanzania

March 2, 2021 12:44 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya makato yasiyo sahihi ya gharama za matumizi ya vifurushi vya simu za mkononi.
  • TCRA imesema imetoa kanuni hizo zitakazoanza kufanya kazi mwezi ujao.
  • Bei za vifurushi vyote zitadhibitishwa na TCRA.

Dar es Salaam. Kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya makato yasiyo sahihi ya gharama za matumizi ya vifurushi vya simu za mkononi, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kanuni mpya za vifurushi zitakazosaidia kutatua changamoto hiyo. 

Waziri wa Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile mwishoni mwaka 2020 aliigiza TCRA kufanyia kazi malalamiko ya muda mrefu yanayotolewa na wananchi dhidi ya kampuni za simu, kuhusu kukatwa au kuibiwa fedha zao kwenye gharama za vifurushi.

Dk Ndungulile alisema mamlaka hiyo inatakiwa kutafuta suluhu ya kudumu ya changamoto hizo. 

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba akitolea tamko suala hilo leo Machi 2, 2021 jijini Dar es Salaam amesema mamlaka hiyo imetengeneza kanuni ndogo za kuratibu utoaji wa huduma za vifurushi vya mawasiliano ya simu.

Kanuni hizo zitasimamia vifurushi vya dakika za kupiga miongoni mwa mitandao ya nchini, bando ya intaneti na meseji. 

Utekelezaji wa kanuni hizo utaanza Aprili 2 mwaka huu ambapo  miongoni mwa yanayoelekezwa kwenye kanuni hizo ni huduma zote za vifurushi lazima zipate vibali vya TCRA ambapo mamlaka hiyo imetoa mwongozo wa bei za vifurushi zinazotakiwa kutekelezwa na kampuni za simu.


Soma zaidi:


Vifurushi vyote vya simu havitaondolewa au kurekebishwa ndani ya miezi mitatu baada ya kuidhinishwa. Pia, mtoa huduma atatakiwa kutoa taarifa kila wakati matumizi ya kifurushi yatakapifikia asilimia 75 kabla ya kuisha na kitakapomalizika kabisa kwa asilimia 100.

Kwa sasa, baadhi ya watoa huduma ukiwemo mtandao wa Airtel, unatoa taarifa ya matumizi ya kifurushi punde kinapotumika kwa asilimia 90 na taarifa ya mwisho baada ya matumizi ya asilimia 100.

Enable Notifications OK No thanks