Netflix kuwavalia njuga wasiolipia akaunti zao

March 13, 2021 10:19 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Imesema ni kwa sababu za kibiashara na kiusalama. 
  • Mtumiaji atatakiwa kuthibitisha akaunti yake kwa njia ya anuani ya barua pepe ambapo atatumiwa neno siri la kuthibitisha.

Dar es Salaam. Kampuni inayosimamia programu tumishi ya simu (App) ya Netflix ya kutazama filamu imeanza kufanya majaribio ya kudhibiti watu wanaotumia akaunti za app hiyo bila kuzilipia.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la The Verge, udhibiti huo utaanza kwa kila mtumiaji wa akaunti ya Netflix kuthibitisha akaunti yake kwa kuiunganisha na anuani ya baruapepe ambayo imesajili akaunti yake. 

Netflix yenye watumiaji zaidi ya milioni 200  imefikia maazimio hayo kwa sababu za kibiashara na kuisalama ili kulinda mapato na taarifa za watumiaji wake zisidukuliwe na watu wenye nia mbaya.


Soma zaidi:


“Endapo mtu atagundulika kuwa anatumia app hiyo bila uhalali, atalazimika kuthibitisha akaunti yake kwa njia ya baruapepe. Neno siri litatumwa katika barua pepe iliyosajilia akaunti hiyo na atalazimika kulithibitisha ndani ya muda fulani. 

Tofauti na hapo, hatoweza kutumia huduma za Netflix,” imeeleza taarifa ya  The Verge kuhusu hatua za Netflix.

Hatua hiyo ni muhimu katika kulifanya jukwaa hilo la filamu za mtandaoni kuwa salama kwa watumiaji wake. Lakini Netflix itakuwa na kibarua kigumu cha kudhibiti matumizi ya neno siri kwa watu zaidi ya mmoja hasa marafiki.  

Pia Netflix  inatakiwa kuzingatia kuwa, wapo watu ambao wamelipia akaunti zao na zinatumiwa na zaidi ya mtu mmoja zikiwemo familia, hivyo inaweza kuwa usumbufu ikiwa kila kifaa kinachotumia akaunti husika kutakiwa kufanya uthibitisho.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
24 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
24 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Nukta TV

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Nukta TV

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Nukta TV