Bashe: Tanzania haitoondokana na matatizo ya kilimo kama haitawekeza katika sekta ya umwagiliaji

April 14, 2021 7:03 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amesema kwa sasa wanafanya mabadiliko makubwa ya mfumo wa Tume ya Umwagiliaji ili itoe tija kwenye kilimo.
  • Amesema kwa sasa Serikali haitajenga miradi mipya ya umwagiliaji mpaka ikamilishe na kuifanyia tathmini iliyopo.

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema katika bajeti ya mwaka 2021/22 wizara yake itaweka mikakati mbalimbali ya kukuza na kuimarisha sekta ya umwagiliaji ikiwemo kubadilisha mfumo wa utendaji wa Tume ya Umwagiliaji (NIC) ili kuondokana na matatizo kilimo  Tanzania. 

Kwa mujibu wa NIC, Tanzania ina hekta milioni 29.4 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ambazo zinaweza kutoa fursa mbalimbali ikiwemo ajira kwa wananchi lakini ni asilimia 1.6 ya ardhi hiyo imeendelezwa, 

Bashe aliyekuwa akizungumza leo Aprili 14, 2021 Bungeni jijini Dodoma amesema sekta ya umwagiliaji haiepukiki katika kukifanya kilimo kiwe na tija kwa wakulima na kuipatia Serikali mapato yatakayosaidia kukuza uchumi wa Taifa. 

“Tanzania haitoondokana na matatizo ya kilimo kama haitawekeza katika sekta ya umwagiliaji,” amesema Bashe ambaye ni Mbunge wa Nzega Mjini.

Amesema ili kuifanya sekta ya umwagiliaji kutoa mchango mkubwa kwenye kilimo ni kubadilisha mfumo wa utendaji wa NIC ili ifanye kazi kwa ufanisi mkubwa kuliko ilivyo sasa. 

“Mbili tunachokifanya kama Serikali ili kutumia vizuri milima ya Usambara na maeneo mengine ya nchi yetu kwa ajili ya kujenga mabwawa,” amesema naibu waziri huyo. 

Pia Wizara ya Kilimo itawekeza katika kununua vifaa vyake yenyewe badala ya kutumia mifumo mingine ili kuongeza kasi ya NIC kujenga miradi ya umwagiliaji na kupunguza gharama za uagizaji vifaa hivyo kutoka nje ya nchi.

“Tutawekeza kununua vifaa wenyewe ili tume ya umwagiliaji iwe na uwezo kwa ajili ya kuchimba mabwawa na kujenga miradi ya umwagiliaji kwa mfumo wa “Force Account” ili kupunguza gharama tunayotumia fedha katika maeneo ambayo tunajenga skimu kubwa,” amesema Bashe.


Soma zaidi: 


Bashe alikuwa akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini Dk Oscar Kikoyo aliyetaka kufahamu Serikali ina mikakati gani ya kukamilisha miradi ya umwagiliaji iliyopo kabla ya kuanzisha mipya.  

Aidha, amesema kwa sasa Serikali haitajenga miradi mipya ya umwagiliaji mpaka ikamilishe na kuifanyia tathmini iliyopo. 

“Kama wizara, kipaumbele chetu cha kwanza sasa hivi tunachokifanya ni kufanya tathmini na kukamilisha miradi ya miradi ya umwagiliaji. Na tathmini tunafanya mbili: moja kuangalia ufanisi wa miradi ya umwagiliaji iliyopo sasa hivi kama inafanya kazi kwa kiwango ambacho kinatarajiwa na kufanya marekebisho pale ambapo tunahitaji kufanya marekebisho.

“Kukamilisha miradi ya umwagiliaji ambayo tumekwisha ianza. Hatutokuja na mradi mpya wa umwagiliaji isipokuwa kukamilisha miradi tuliyoianza,” amesisitiza.

Huenda, mikakati hiyo ikawasaidia wakulima ambao wana maono ya kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji ili wafaidike na fursa zilizopo kwenye sekta hiyo. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV