Kubali matokeo, fungua ukurasa mpya wa maisha

April 27, 2021 1:24 pm · Neema
Share
Tweet
Copy Link
  • Siyo kila kitu unapaswa kukomaa nacho kwenye maisha.
  • Vingine viache na anza upya kujenga maisha yako. 

Umewahi kuwa katika wakati mgumu ambao huelewi utatoka vipi ama utafanya  nini? Umefika mwisho wa hekima ya kufanya mambo yako?

Ulifanya nini kutoka katika mkwamo huo? Hayo ni baadhi ya maswali ambayo kila tunapopitia kwenye changamoto fulani ya maisha huja kichwani.

 Zipo changamoto ambazo unaweza kuzipatia ufumbuzi na ukatoboa lakini zingine zinahitaji ukubali matokeo yaani utafute mwelekeo mwingine.

Siyo kila ulichopanga kitaenda vile unavyotaka, zipo ajali mbalimbali za maisha zinazoweza kutokea. Mfano, ukifiwa na mume au mke wako mpenzi huwezi kumrudisha tena, unatakiwa kukubali matokeo na kuendelea na maisha ya ujane au ugane.

Baada ya kukubali matokeo ya kile kilichotokea, usikumbuke tena ya nyuma, nenda na mweleko mpya wa maisha. Fungua ukurasa mpya na pigani kesho yako nzuri.

Huenda umetapeliwa, umepoteza marafiki au watu muhimu katika maisha yako na umeanza kukataa tamaa ukiamini maisha bila wao hayawezekani. Hapana inawezekana maana kila linalotokea kwenye maisha lina funzo na fursa mpya ya kukufanya uwe bora zaidi.

Anza hapo ulipokwama kuiendea safari mpya ya maisha yako. Bado una nafasi ya kubadilisha maisha yako yakawa mazuri zaidi ya sasa.

                                 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW