Serikali kufanya mapitio mitaala shule za msingi, sekondari

April 30, 2021 6:24 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Mapitio hayo yatafanyika mwaka 2021/22.
  • Katika mitaala hiyo zitaingizwa stadi za maisha na mbinu tete.
  • Stadi hizo zitawasaidia wahitimu kuwa na uwezo wa kiushindani katika soko la ajira. 

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema inakusudia kufanya mapitio ya mitaala ya shule za msingi na sekondari ili kuingiza stadi mbalimbali za maisha zitakazowasaidia wahitimu kuwa na uwezo wa kiushindani katika soko la ajira. 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga amesema Serikali inatambua umuhimu wa kuwawezesha wanafunzi kupata stadi mbalimbali ikiwemo stadi za maisha na tete ili kuwa uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo suala la ajira.

“Katika kipindi cha mwaka fedha 2021/22 Serikali itafanya mapitio ya mitaala shule za msingi na sekondari ili kuingiza stadi mbalimbali kama vile stadi za maisha, stadi za karne ya 21 na mbinu tete,” amesema Kipanga leo Aprili 30, 2021 bungeni jijini Dodoma.

Stadi za karne ya 21 ni pamoja na fikra tunduizi, ubunifu, ushirikiano, uongozi na stadi za teknolojia ya habari na mawasiliano.


Zinazohusiana:


Kipanga ambaye ni Mbunge wa Mafia amesema mapitio hayo yanafanyika kutokana na kuwepo kwa mahitaji ya soko la ajira yanayotokana na mabadiliko ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kiteknolojia duniani. 

Naibu Waziri huyo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Nusrat Hanje ambaye alitaka kufahamu Serikali  inafanya nini kuwapatia wanafunzi stadi za maisha na mbinu tete (soft skills) ili kumudu mahitaji na ushindani wa soko ajira.

“Serikali haioni haja ya kurekebisha mfumo wa elimu na kuingiza mbinu tete na stadi za maisha ili kuwajengea uwezo wakiushindani vijana wanaohitimu kupunguza tatizo la ajira,” ameuliza Hanje katika swali lake. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
4 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
4 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

Nukta TV

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

Nukta TV

Nukta Africa ndani ya Africa Agri Expo 2026

Nukta Africa ndani ya Africa Agri Expo 2026

Nukta TV