Rais Samia: Uamuzi wangu wa kuja Kenya si wa bahati mbaya

May 5, 2021 12:23 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amesema hiyo ndiyo ziara yake ya kwanza tangua aingie madarakani Machi 19 mwaka huu. 

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema ziara yake nchini Kenya iliyoifanya kwa siku mbili ndiyo ziara yake kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Rais wa sita wa Tanzania Machi 19 mwaka huu. 

Rais Samia amebainisha hayo leo Mei 5, 2021 jijini Nairobi wakati akihutubia kikao cha Bunge la Taifa na Seneti na kueleza kuwa alitembelea Uganda hivi karibuni lakini haikua ziara rasmi.

“Uamuzi wangu wa kuja Kenya si wa bahati mbaya bali ni wa makusudi, busara inaelekeza kuwa ukiwa mpangaji mpya kwenye eneo ni lazima ujitambulishe kwa majirani, nilipata mialiko mingi lakini nikasema nianze hapa,” amesema Rais Samia na kubainisha kuwa Kenya na Tanzania ni ndugu na zina ushirikiano wa muda mrefu ambao hauwezi kuyumbishwa na mtu yeyote. 

Amesema Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kwa Kenya  huku akizitaka nchi hizo mbili kuziona kama ndugu na siyo washindani ambao wanaishi kwa kuhasimiana. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
19 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
19 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
19 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV