Jinsi ya kunyoa nywele za sehemu za siri kwa usahihi

May 29, 2021 8:05 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Kunyoa nywele za sehemu za siri siyo lazima, ni chaguo la mtu binafsi.
  • Safisha zana unayotumia na kujua ueleekeo wa ukuaji wa nywele.

Dar es Salaam. Baadhi ya watu hulalamika kuwa na vipele, muwasho katika sehemu za siri na ni ukweli usiopingika kuwa baadhi yao hupata changamoto hiyo baada ya kushindwa kunyoa nywele za sehemu za siri kwa ufasaha pale zinapokuwa zimerefuka.

Kushindwa kukata nywele hizo kwa usahihi kunaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa ikiwemo magonjwa ya ngozi na fangasi.

Kwa kawaida, kunyoa nywele za sehemu za siri inahitaji zana sahihi ya kunyolea na huduma ya ngozi yako baada ya kumaliza.

Hata hivyo, mtaalamu wa afya Dk Joshua Sultan amesema suala la kunyoa sehemu za siri ni suala binafsi na kila mtu ana mapendeleo yake.

“Baadhi hupendelea kufuga na kuziacha zikue sana na baadhi hupendelea kimo kifupi na wengine huondoa kabisa. Kuziondoa kabisa huweza kupelekea msuguano na uwezekano wa vijidudu na uchafu kuingia kwa urahisi zaidi,” ameandika Daktari huyo katika ukurasa wake wa Twitter.

Je, kama wewe umechagua kunyoa nywele hizo, uzingatie nini ili kuepukana na adha za kiafya zinazoweza kutokea? Tazama video hii kujifunza.

Enable Notifications OK No thanks