Siri shule iliyoongoza ufaulu masomo ya lugha, sanaa kidato cha sita

July 17, 2021 6:24 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni shule ya Dareda ya mkoani Manyara iliyoshika nafasi ya tatu kitaifa.
  • Imeongoza kitaifa ufaulu masomo ya kugha na sanaa.

Dar es Salaam. Shule ya Sekondari Dareda inaweza ikawa ngeni kwenye baadhi ya masikio ya watu lakini mwaka huu huenda ikasikika zaidi.

Hiyo inatokana na kufanya vizuri katika  matokeo ya kidato cha sita mwaka 2021 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta).

Shule hiyo iliyopo mkoani Manyara,kwa mujibu wa Necta imeshika nafasi ya tatu kitaifa huku ufaulu wa wanafunzi wake ukikomea daraja la I na II.

Matokeo hayo mazuri ya mwaka huu iliyopata Dareda siyo bahati mbaya. Imekuwa na ufaulu mzuri tangu mwaka 2019 na katika kipindi hicho wanafunzi wake hawajawahi kupata ufaulu wa daraja la sifuri wal IV.

Kilichoibua mjadala kwa shule hiyo ya Serikali ni wanafunzi nane kati ya 10 waliofanya vizuri katika masomo ya lugha na sanaa (arts) ya mwaka wametoka katika shule hiyo. 

Katika orodha ya wavulana 10 waliofanya vizuri zaidi kitaifa katika masomo ya sanaa na lugha, nane wametoka Dareda huku ingiiza wasichana wawili wakiingia 10 bora ya wasichana waliofanya vizuri katika masomo hayo.

Pia imeshika nafasi ya kwanza kitaifa kwa ufaulu wa masomo hayo ya lugha na sanaa ambayo hujumuisha Historia, Jiografia, Kiingereza, Kiswahili na General Studies (GS).

Dareda ambayo ni shule ya Serikali imejibebea umaarufu mkubwa katika matokeo ya kidato cha sita 2021 kwa sababu kuzipiga kikumbo shule za binafsi katika ufaulu. Picha| Saangapi Tv.

Safari ilianza mdogo mdogo

Kwa Dareda kufikia nafasi ya tatu kitaifa na kuongoza masomo yote ya sanaa huku ikitawala orodha ya 10 bora ya wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya sanaa na lugha, ilianza kujipanga kwa muda mrefu.

Kwa mwaka 2019, shule hiyo iliyoshika nafasi ya 16 kitaifa, ufaulu wa masomo yake ya sanaa uliangukia kwenye nafasi ya 40 kitaifa. 

Mwaka huo Dareda ilishika nafasi ya 39 katika somo la historia, Jiografia (15), Kiingereza (14) na nafasi ya 10 katika somo la Kiswahili.

Mapinduzi yalionekana mwaka 2020 ambapo ufaulu wake kimasomo uliiwezesha kuingia katika orodha ya shule 20 zilizofanya vizuri kimasomo.

Mwaka jana katika somo la Kiingereza, Kiswahili (7) na nafasi ya tatu kwa masomo ya Historia na Jiografia.

Kwa mwaka huo, hata masomo ya sayansi ilifanya vizuri ikiwa nafasi ya 17 somo la Baiolojia na nafasi ya 35 somo la Kemia.

Katika ufaulu ndani ya mkoa wake inafanya vizuri. Tangu mwaka 2019, shule hiyo imekuwa ikishika nafasi ya kwanza katika mpangilio wa ufaulu wa shule ndani ya Mkoa wa Manyara na kuzibwaga shule za binafsi.

Shule hiyo inatoa elimu kwa michepuo mitatu yaani HGL (Historia, Jiografia na Kiingereza), HKL (Historia, Jiografia na Kiingereza) na CBG (Kemia, BaIolojia na Jiografia).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV