Jinsi ya kukomesha uonevu, unyanyasaji wa mtandaoni kwa watoto

February 14, 2022 3:01 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Marafiki wote hutaniana wao kwa wao, lakini wakati mwingine ni vigumu kujua ikiwa mtu anafurahia utani huo au unamuumiza. 

Februari 8 mwaka huu ilikuwa Siku ya Mtandao Salama duniani. Wadau mbalimbali walijadili na kutoa mapendekezo mbalimbali ya namna ya kuzuia na kukomesha unyanyasaji na uonevu mtandaoni hasa kwa watoto. 

Hata hivyo, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) linatambua kuwa dunia ipo katika wakati ambao mtandao unaenea karibu kila nyanja ya maisha.

Kutokana na ukweli huo wazazi, walezi na walimu wamebeba jukumu la kuhakikisha watoto na vijana wako salama mtandaoni kwa kuwa utafiti uliofanywa na Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano ( ITU) ulibainisha kuwa vijana hutumia muda mwingi mtandaoni kuliko umri mwengine.

Utafiti huo wa mwaka 2020, umewaonesha kuwa na uwezekano wa vijana kuunganishwa kwenye mtandao kwa asilimia 24 kuliko watu wengine wote. 

Pia inakadiriwa kuwa asilimia 71 ya vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 na 24 wanatumia intaneti, ikilinganishwa na asilimia 57 tu katika makundi mengine ya umri.

Miongoni mwa masuala yanayoumiza vichwa wazazi na walezi wengi ni suala la watoto kuonewa au kunyanyaswa mtandaoni ”cyberbullying“ na ndio maana UNICEF katika kuadhimisha siku hiyo ya mitandao salama imekuja na mbinu kadhaa za kuelimisha namna ya kupambana na hali hizo hususan kwa watoto. 

Watoto wasichana wakifuatilia taarifa kwa kutumia simu za mkononi. Picha| UNICEF/Estey.

Masuala 7 ambayo yanaweza kusaidia kumaliza unyanyasaji wa watoto mtandaoni ambayo UNICEF imependekeza:

1. Uonevu wa mtandaoni ni nini?

Uonevu mtandaoni ni unyanyasaji unaotendeka kwa kutumia teknolojia za kidijitali. Mtu anaweza kufanyiwa kwenye mitandao ya kijamii, majukwaa ya kutuma ujumbe, majukwaa ya michezo ya kubahatisha na hata kwenye simu za mkononi. 

Uonevu huu huwa na tabia ya kujirudia, lengo likiwa ni kutisha, kukasirisha au kuwaaibisha wale wanaolengwa. 

Mifano ya matendo ya uonevu wa mtandaoni ni pamoja na kueneza uwongo, kutuma picha au video za aibu za mtu fulani kwenye mitandao ya kijamii. Kutuma ujumbe, picha au video za kuumiza, matusi au vitisho kupitia mifumo ya ujumbe, kuiga mtu mwingine na kutuma ujumbe mbaya kwa wengine kwa niaba yao au kupitia akaunti za kughushi.

Uonevu wa ana kwa ana na ule wa mtandao mara nyingi unaweza kutokea pamoja. Lakini uonevu mtandaoni huacha alama za kidijitali , na hizi kuweza kutumika kama rekodi muhimu ya kutoa ushahidi wa kusaidia kukomesha uonevu huo.

 

3. Unawezaje kutofautisha mzaha na uonevu mtandaoni?

Marafiki wote hutaniana wao kwa wao, lakini wakati mwingine ni vigumu kujua ikiwa mtu anafurahia utani huo au unamuumiza. Wakati mwingine mtu anaweza kukuumiza nafsi na kuishia kucheka kwa kusema “natania tu,” au “usiichukulie kwa uzito sana.”

Ikiwa unahisi kuumia au kufikiria wengine wanakucheka, basi mzaha huo umekwenda mbali sana na ni vyema kumwambia anayefanya hivyo aache mara moja. Ikiwa ataendelea hata baada ya kumwomba, basi huu unaweza kuwa uonevu.

Na hali huwa mbaya zaidi inapofanyika mtandaoni kwa sababu watu wengi wanaona wakiwemo wageni. Ikiwa huna furaha kuhusu jambo hilo, hupaswi kukaa kimya. Na ikiwa unajisikia vibaya ni vyema kupata msaada. 

Kukomesha uonevu wa mtandao siyo tu kuwataja wakorofi, bali pia ni kutambua kwamba kila mtu anastahili heshima mtandaoni na katika maisha halisi.

Nchini Ufaransa, hatari ya utoro ni mara tatu zaidi kati ya waathiriwa wa unyanyasaji wa mtandao. Picha| Anthony Tran/Unsplash

4. Madhara ya uonevu mtandaoni

Madhara yanaweza kudumu kwa muda mrefu na kuathiri mtu kwa njia nyingi:- Kiakili kwa kujisikia hasira, aibu, mjinga, hofu au hasira; Kihisia (kujisikia aibu au kupoteza hari ya kufanya mambo unayopenda); na Kimwili  kwa uchovu (kukosa usingizi), au kupata dalili kama vile maumivu ya tumbo na maumivu ya kichwa.

Hisia ya kuchekwa au kunyanyaswa na wengine, inaweza kuzuia watu kuzungumza au kujaribu kushughulikia tatizo linalowakabiili. Katika hali mbaya zaidi, uonevu wa mtandao unaweza hata kusababisha watu kujiua.

Uonevu  mbali na kuleta athari nyingi lakini aliyefanyiwa vitendo hivyo anaweza kushinda hisia mbaya na kurejesha imani na afya yake.

5. Nimfuate nani iwapo nimefanyiwa uonevu mtandaoni?

Ni muhimu sana kutoa ripoti iwapo umefanyiwa uonevu mtandaoni.  

Hatua ya kwanza ni kutafuta msaada kutoka kwa mtu unayemuamini kama vile wazazi wako, rafiki yako, mwanafamilia au mtu mzima mwingine unayemuamini.

Ikiwa ni shuleni unaweza kuwasiliana na mshauri, mkufunzi wa michezo au mwalimu unayempenda, na unaweza kufanya hivi kwa njia ya mtandao au ana kwa ana.

Na ikiwa huna raha kuzungumza na mtu unayemjua, tafuta simu ya usaidizi katika nchi yako ili kuzungumza na mshauri wa kitaalamu.

Ikiwa uonevu unafanyika kwenye mtandao wa kijamii, zingatia kumzuia mnyanyasaji na kuripoti rasmi tabia zao kwenye mtandao huo. Makampuni ya mitandao ya kijamii yana wajibu wa kuwaweka watumiaji wao salama.

Ili kukomesha uonevu ukome, inahitaji kutambuliwa na kuripotiwa.

Kusanya na hifadhi ushahidi, iwe ni  ujumbe mfupi au picha za simu , upige picha “screenshot” ili kuonyesha kile ambacho kimekuwa kikiendelea.

Ili uonevu ukome, inahitaji kutambuliwa na kuripoti ni muhimu. Inaweza pia kusaidia kuonyesha mnyanyasaji kwamba tabia yake haikubaliki.

Ikiwa uko katika hatari na unahitaji jambo hilo kutatuliwa kwa dharura basi unapaswa kuwasiliana na polisi au huduma za dharura katika nchi yako.


Soma zaidi: 


6. Jinsi ya kumsaidia rafiki aliyeonewa mtandaoni

Mtu yeyote anaweza kuwasilisha taarifa za unyanyasaji wa mtandaoni. Ukiona mtu anatendewa vitendo viovu na unamfahamu jaribu kutoa usaidizi.

Ni muhimu kumsikiliza rafiki yako au mtu huyo kwanini anaogopa kwenda kutoa taarifa na kuonewa mtandaoni. Unaweza kumuuliza Je, wanajisikiaje? 

Unaweza kumsaidia kwa kumjulisha kwamba si lazima aripoti chochote rasmi, lakini ni muhimu kuzungumza na mtu ambaye anaweza kusaidia.

Zingatia;- 

Rafiki yako anaweza kuwa na hisia dhaifu. Kuwa mkarimu kwake , msaidie kufikiria anachoweza kusema. Jitolee kwenda naye ikiwa ataamua kwenda kutoa malalamiko rasmi. Muhimu zaidi, mkumbushe kuwa uko kwa ajili yake na unataka kumsaidia.

Ikiwa rafiki yako bado hataki kuripoti tukio hilo, basi umuunge mkono kutafuta mtu mzima anayemwamini ambaye anaweza kumsaidia kukabiliana na hali hiyo. Kumbuka kwamba katika hali fulani matokeo ya unyanyasaji mtandaoni yanaweza kutishia maisha.

Kutofanya chochote kunaweza kumfanya mtu ahisi kwamba kila mtu yuko kinyume naye au kwamba hakuna anayejali. Maneno yako yanaweza kuleta mabadiliko.

Kampuni za mitandao ya kijamii zina sera na kanuni za kuzuia unyanyasaji mtandaoni. Picha| Unsplash/Solen Feyissa

7. Zana za kuzuia unyanyasi na uonevu mtandaoni kwa vijana

Kila mtandao wa kijamii hutoa zana tofauti zinazokuruhusu kuweka vikwazo kuhusu nani anayeweza kutoa maoni au kutazama machapisho yako au anayeweza kuunganishwa kama rafiki, na kuripoti visa vya uchokozi. 

Nyenzo nyingi kati ya hizo zinahusisha hatua rahisi za kuzuia, kunyamazisha au kuripoti unyanyasaji wa mtandaoni. 

Kampuni za mitandao ya kijamii pia hutoa elimu na mwongozo kwa watoto, wazazi na walimu kujifunza kuhusu hatari na njia za kukaa salama mtandaoni.

Kumbuka ya kwanza ya ulinzi dhidi ya uonevu mtandaoni inaweza kuwa wewe mwenyewe. Fikiria kuhusu mahali ambapo unyanyasaji wa mtandaoni hutokea katika jumuiya yako na njia unazoweza kusaidia  kwa kupaza sauti yako, kuwataja waonevu, kuwasiliana na watu wazima unaowaamini au kwa kutoa ufahamu kuhusu suala hilo. 

Kama umeshawahi kufanyiwa uonevu mtandaoni haupo peke yako , tazama video hii ya vijana waliofanyowa uonevu ambao wanaeleza namna uya kukabiliana na hali hiyo. 

Enable Notifications OK No thanks