Ushindani; Nissan warejea sokoni na gari jipya

May 27, 2022 10:15 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya kupita katika kipindi kigumu cha ushindani.
  • Litauzwa kuanzia Sh72 milioni.

Dar es Salaam. Hii inaweza kuwa habari njema kwa wapenzi wa magari mara baada ya kampuni ya utengenezaji na uuzaji wa magari ya Nissan iliyopo nchini Japan kutangaza kuingiza gari jipya sokoni.

Gari hilo Nissan 350Z ni toleo la sita ambalo kwa sasa linaitwa Nissan 370Z.

Toleo kwanza la Nissan Z ilikuwa ni Datsun 240Z iliyotolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1969 huko nchini Marekani na kufanya vizuri katika mataifa ya Asia na Marekani Kaskazini. 

Toleo hilo liliboreshwa na kuja na matoleo mapya kama 260Z na 280Z iliyotoka mwaka 1980.

Nissan waliendelea kutoa matoleo mbalimbali ya Nissan Z na kufikia mwaka 2003 waliachia toleo la tano la Nissan Z iliyoitwa Nissan 350 Z ikiwa imeboreshwa zaidi ambapo ilifanya vizuri sokoni kwa karibu nusu muongo.

Toleo la mwisho la Nissan 370 Z lilibuniwa mwaka 2009 na lilikuwa sokoni mpaka mwaka 2020 ambapo halikuwahi kufanyiwa maboresho yoyote.

Toleo la mwisho la Nissan 350Z iliyotoka mwaka 2009. Picha|Nissan

Kampuni ya Nissan ilikuwa katika kipindi kigumu kwa muda wa miaka mitano tangu alipokamatwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Carlos Ghon akiwa  nchini Japan kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya ofisi, jambo lililosababisha kuvuliwa ukurugenzi na uanachama wa kampuni hiyo. 

Mkuu wa ubunifu wa Nissan Alfonso Aldaisa alinukuliwa na vyombo vya habari akisema walikuwa kwenye kipindi kigumu kwani mkurugenzi aliyepita alikuwa anazingatia zaidi kuuza kuliko takwa la mteja.

“Muda wote tulikuwa tunahangaika kujua sisi ni kina nani kama kampuni, hata mimi nilichanganyikiwa,nilikuwa na msongo wa mawazo,” alisema Albaisa.

Toleo hilo jipya la Muundo wa 370Z linategemewa kufanya vizuri sokoni na kuirudisha kampuni ya Nissan katika ramani ya kibiashara tangu kuporomoka kwake mwaka 2018.  

Gari hiyo itaingizwa rasmi sokoni kuanzia mwezi September mwaka huu ambapo itakugharimu Dola za Marekani 31,000 (Sh72 milioni) kwa toleo la kawaida wakati toleo la Nissan 370Z sports litauzwa kuanzia Dola za Marekani 50,000 sawa na Sh116 milioni.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW