Sababu Tanesco kusitisha huduma za kununua Luku kwa saa mbili

June 7, 2022 10:57 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kuboresha mfumo wa manunuzi ya umeme kwa njia ya luku.
  • Maboresha hayo yatasaidia kuongeza ufanisi wa mifumo ya shirika hilo.

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema huduma ya kununua umeme kupitia Luku itakosekana kwa muda wa masaa mawili usiku kuamkia Alhamisi Juni 9 mwaka huu ili kupisha matengenezo ya mifumo yake.

Tanesco imetoa taarifa hiyo kupitia Meneja Mwandamizi wa Tehama Cliff Maregeli alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Juni 6 makao makuu ya Tanesco Jijini Dar es Salaam

‘Tunategemea kwamba kwa muda wa masaa mawili kuanzia saa sita usiku mpaka saa saba hivi, wateja hawataweza kununua umeme wakati tukiwa tunafanya matengenezo,” amesema Maregeli.

Tanesco imewataka wateja wake kununua umeme wa ziada ili kuepuka usumbufu wowote utakaoweza kujitokeza au hata kama ikitokea hitilafu yoyote waweze kustahimili  wakati wanafanya matengenezo.

Matengenezo hayo yatafanyika kati mifumo ya kuuza umeme kwa ulipaji wa kabla yaani Luku, katika kituo cha kujikinga na majanga. 

Pia yataliweka shirika katika hali nzuri ya kuhimili hitilafu yoyote itakayoweza kujitokeza kwenye mfumo wa manunuzi. 

Sambamba na hilo matengenezo hayo yataongeza utayari wa kuwahudumia wateja pale itakapotokea hitilafu katika mfumo mkuu kwa sababu watakuwa na seti mbili za mifumo zitakazowawezesha wateja kupata huduma endelevu.


Soma zaidi:


Wananchi wameipokeaje taarifa hii?

Patrick Kanayoge mkazi wa kunduchi, jijini Dar es Salaam, ameshukuru shirika hilo kutoa taarifa ya kukokesakana kwa huduma hiyo kwani wananaweza kujipanga mapema.

“Nashukuru kupata taarifa hii mapema nitanunua umeme wa kutosha kabla ya siku ya jumatano,” amesema Kanoyoge huku akitaka utaratibu huo uwe unafanyika hata wanapotaka kukata umeme.

Hata hivyo, baadhi ya watu hawajapa taarifa hiyo, jambo linaloweza kuwasababishia hasara katika biashara zao endapo hawatanunua umeme wa kutosha.

“Hapa itabidi tu tujipange mapema ikiwezekana tutafute jenereta la ziada ili ikishindikana  kupata umeme tunaliwasha nyama zisioze,” mesema Jamal Husein, muuza bucha Mwananyamala.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii akiwemo Rahma Chingwile anayetumia Instagram ameuliza “ Mlisema kuanzia Julai 2022 tutakuwa tunanunua umeme kama tunavyonunua kwa ving’amuzi, mmefikia hatua gani?”

Naye Royal Soldier kutoka mtandao wa instagram anasema ikiwa maboresho hayo yatafanikiwa itawarahisishia ununuzi wa umeme kwa njia yenye ufanisi zaidi,

“Nilikuwa nausubiri kwa hamu sana huu mfumo. Mungu awaongoze katika kufanikisha hili,” amesema Solder wakati akitoa maoni yake. 

/
No matches found for this filter
30 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV