Matokeo kidato cha sita 2022 yatangazwa, ufaulu waongezeka kidogo

July 5, 2022 2:23 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Kaimu Katibu wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) , Athuman Amas akitangaza matokeo ya kidato cha sita na ualimu kwa mwaka 2022. Picha| Jesse Mikofu.


  • Ufaulu wa jumla kwa watahiniwa wa shule ukiongezeka kidogo kwa asilimia 0.25.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) leo limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita huku ufaulu wa jumla kwa watahiniwa wa shule ukiongezeka kidogo kwa asilimia 0.25.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amas akitangaza matokeo ya kidato cha sita na ualimu kwa mwaka 2022 leo Julai 5 visiwani Zanzibar amesema ufaulu wa jumla kwa watahiniwa hao wa shule umeongezeka hadi asilimia 99.87 mwaka huu kutoka asilimia 99.26 mwaka jana.

“Tathmini ya awali ya matokeo haya, unaonyesha ufaulu wa jumla wa watahiniwa wa shule katika mtihani wa kidato cha sita uliofanyika Mei 2022 umepanda kidogo kwa silimia 0.25,” amesema Amas.

Necta imesema watahiniwa 93,136 wa shule na kujitegemea wamefaulu mitihani hiyo kati ya watahiniwa 94,456 waliofanya mitihani hiyo ya kumaliza kidato cha sita Mei mwaka huu.

Ufaulu huo wa jumla wa wanafunzi wa shule na kujitegemea ni sawa na asilimia 99.87 ya wanafunzi wote waliofanya mitihani hiyo ambayo ni daraja muhimu kujiunga na elimu ya juu.

Ufaulu huo wa mwaka 2022 umeshuka kwa asilimia 0.09 ikilinganishwa na asilimia 99.06 ya mwaka jana.

Kati ya waliofaulu, wavulana  walikuwa 52,229 sawa na asilimia 98.55 ya watahinjiwa waliosajiliwa.

Kwa mujibu wa Necta, watahiniwa 95,826 walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu ambapo 41,571 (asilimia 43.33) walikuwa ni wasichana.

Hata hivyo, watahiniwa 94,456 sawa na asilimia 98.57 ya watahiniwa wote waliosajiliwa walifanya mtihani huo.


Soma zaidi: 


Ubora wa ufaulu

Kuhusu ubora wa ufaulu kwa mpangilio wa madaraja, Amas amesema jumla ya watahiniwa 83,877 sawa na asilimia 99.24 ya watahiniwa wote wamepata daraja la I hadi III. Kati yao wasichana ni 37,170.

Masomo ambayo ufaulu umeongezeka ukilinganisha na mwaka jana ni History, French, English, Arabic, Physics, Agriculture, Biology, Accountancy, Advanced Mathematics na Food and Human Nutrition.

“Ufaulu katika soko la Commerce ni asilimia 99.85 sawa na ufaulu wa mwaka 2021. Ufaulu katika somo la Kiswahili ni asilimia 100 sawa na 2021. 

“Aidha, ufaulu katika masomo ya General Studies, Geography, Basic Applied Mathematics na Computer Science umeshuka ukilinganisha na mwaka 2021,” amesema kaimu katibu mtendaji huyo wa Necta.

Enable Notifications OK No thanks