Ifahamu mashine ya kienyeji inayotumika kuyeyusha vyuma makaburini

July 16, 2022 6:31 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ally Kisukari alibuni mashine hiyo miaka 10 iliyopita.
  • Mashine hiyo inatumia mfumo wa kiyoyozi cha gari (AC).
  • Mashine hiyo hengeneza misumari 100 hadi 200 kwa siku.

Dar es Salaam, Ndani ya banda dogo chakavu pembezoni mwa makaburi mashuhuri ya Mwananyamala mmoja wa wafua vyuma yupo ‘bize’ akiyeyusha vyuma kwa kutumia mashine ndogo iliyotengenezwa kienyeji. 

Mashine hiyo ya umeme, ambayo bado haijapewa jina rasmi, kazi yake kubwa ni kuzalisha upepo ili kuwasha mkaa unaotumika kuyeyusha vyuma na kutengeneza bidhaa mbalimbali za uhunzi.

Ubunifu wa mashine hiyo iliyofanywa na kijana Ally Kisukari miaka 10 iliyopita ulitokana na kukosa fedha za kununua mashine za kisasa ili kujiajiri katika shughuli za uhunzi. 

“Hii mashine inanisaidia sana kutengeneza misumari kwa sababu moto wa mkaa unawaka wakati wote…hapa naweza kutengeneza misumari 100 hadi 200, na kila mmoja nauza 350,” anasema Ally anayefanya kazi za uhunzi Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Kwa kawaida, mashine ndogo za kisasa ambazo zingefaa kumsaidia Ally kufanya shughuli zinauzwa wastani wa Dola za Marekani 7,000 mpaka 9,000 sawa na Sh16.1milioni mpaka Sh20.7 milioni. 

Mashine ya kina Ally  imetengenezwa kwa  bomba maalum la chuma lililochomelewa na kutengeneza tundu dogo linalotoa upepo huku ndani ya chuma hilo kukiwa na mfumo wa kiyoyozi cha gari (AC) ambao umeunganishwa na umeme wa kawaida.

Mfumo huo huzalisha upepo kwa ajili ya kuwasha moto wa mkaa ili kuwa kuhakikisha kuwa mkaa huo umekolea wakati wote anapokuwa analainisha vyuma mbalimbali anavyotengeneza. 

Ally Kisukari, mhunzi akiyeyusha chuma kwa kutumia mashine yake ya kienyeji pembezoni mwa makaburi ya Mwananyamala kwa Kopa. Picha|Daudi Mbapani.

Wazo la kubuni mashine lilitokea wapi?

Wazo la kubuni mashine  hiyo  lilianza  miaka 17  iliyopita, wakati alipoanza kufanya kazi za uhunzi, miaka saba baadae alifanikiwa kutengeneza mashine hiyo kwa kushirikiana na wenzake.

“Huko zamani tulikuwa tunatumia ngozi za wanyama kama Ng’ombe, au Mbuzi, baadae tukawa tunatumia mipira ya magari, tunaisaga na kukausha kisha tunatumia,” anasema Ally aliyefundishwa ujuzi huo na baba yake. 

“Tulipopata tu akili hiyo tukaenda dukani tukanunua mfumo wa kiyoyozi cha gari, tukaja tukafikiria namna mashine yetu itakavyofanya kazi ndipo tukapata wazo la kuunganisha mabati na kutengeneza jumba la nje,” anaongeza. 


‘Mashine hiyo ni noma’

Mashine hiyo ina uwezo wa kufanya kazi kwa saa 12 mfululizo, hata hivyo, huwashwa kwa muda mchache ili kuchochea moto na kisha huzimwa wakati vyuma vimeshayeyuka. 

Mashine hiyo ya kufua vyuma hutumia umeme kama zilivyo mashine nyingine na Ally hutumia umeme wa Sh10,000 kwa mwezi ili kufanikisha shughuli zake za utengenezaji wa misumari ya kutengeneza majeneza na mitumbwi kupitia mashine hii.

Ally anasema kazi ya mashine hii ni kuchochea moto wa mkaa unaotosha kuyeyusha chuma hivyo inamlazimu kununua chenga za mkaa wa Sh1,000 kwa debe na kuwasha moto anaoutumia kuyeyusha vyuma vyake.


Soma zaidi: 


Utunzaji wa mashine 

Katika eneo lake la kazi amejenga kibanda  kidogo chenye upana wa futi tano japo ni chakavu lakini anahakikisha hakipitishi maji yanayoweza kuleta hitilafu katika mashine hiyo. 

“Umeme na maji hauendani, tumetengeneza banda vizuri ili mashine isiingie maji wala kunyeshewa, pia isije ikapata kutu, amesema  Ally.

Tangu kubuniwa kwa mashine hiyo imewahi kuharibika mara moja tu, ambapo ikiharibika inawabidi kubadilisha mfumo wa ndani wa A/C ambao wanaweza kununua dukani kwa Sh70,000, au kwenye magari chakavu na yaliyopata ajali  kwa Sh30,000.


Tangazo:


Wateja wasifu ubora wa bidhaa zake za kienyeji

Gabinus Mussa, mfanyabiashara katika soko la vinyago Mwenge jijini Dar es Salaam ambaye hununua bidhaa za Ally anakiri patasi anazotengeneza Ally zimekuwa zina ufanisi mkubwa katika kazi yake ya uchongaji. 

“Mimi huwa sipendi kwenda dukani, napendelea kuja hapa (kibanda cha Ally) kwa sababu vifaa hivi anavyotengeneza Ally ni imara na bei rahisi,” anasema Ganinus wakati akitoka kununua patasi kwa mhunzi huyo. 

Baadhi ya wajasiriamali wanaofanya kazi kando ya banda la Ally wanampongeza kwa kubuni teknolojia hiyo kwa kuwa wanaona jinsi inavyo msaidia kufanya kazi kwa haraka.

Licha ya kijana huyo mwenye familia ya watoto watatu kujibidiisha katika kazi yake, bado hajafanikiwa kuifanya biashara yake kuwa ya kisasa kutokana na kutumia mashine duni ya kutengeneza vifaa hivyo.

Teknolojia anayotumia Ally humfanya kutumia nguvu nyingi za mwili na muda mrefu kukamilisha majukumu yake tofauti na ambavyo angetumia mashine za kisasa. 

Hata hivyo, ally anasema yupo tayari kubuni mashine nyingine bora zaidi na kama ipo tayari imeshabuniwa yupo tayari kuitumia ili kazi yake iwe nyepesi zaidi.

/
No matches found for this filter
30 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV