Benki ya NBC kuongeza tija kilimo cha Tanzania

August 5, 2022 12:26 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Kuwafikia wakulima wengi kwa pembejeo za kilimo.
  • Kuwasaidia kuongeza uzalishaji na kipato.
  • Kuwapatia bima wakulima ili kufidia majanga.

Dar es Salaam. Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesema inatarajia kuongeza tija katika sekta ya kilimo kwa kuwafikia wakulima wengi zaidi kwa pembejeo bora ili kuongeza uzalishaji na mapato katika shughuli zao.

Benki hiyo imesema inatekeleza lengo hilo kupitia mradi wake wa “NBC Shambani” kwa ushirikiano na makampuni za pembejeo kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini Tanzania.

Raymond Urassa, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Wadogo Wadogo akizungumza Agosti 4, 2022 katika maonyesho ya wakulima ya Nane Nane mkoani Mbeya amesema benki hiyo haitawaacha nyuma wakulima wa Tanzania.

“Tumejipanga kuwahudumia wote walio katika mnyororo wa thamani kuanzia wazalishaji mpaka wachakataji mazao. Wakulima wadogo wadogo, wasafirishaji wa mazao, wasambazaji wa bidhaa na pembejeo kuhakikisha huduma bora kwa wakulima,” amesema Urassa.


Soma zaidi:


Benki hiyo inashirikiana na makampuni mbalimbali ikiwemo Agricom na ETC kutoa pembejeo na zana bora za kilimo kama mashine za uvunaji, matrekta, power tiller kuchochea uzalishaji wenye tija.

Amesema wamejipanga kutanua wigowa kuwafikia wakulima hasa wadogo ili kuwajengea uwezo wa kuzalisha kwa faida. 

“Kuhusu wazalishaji wadogo benki inashughuka na mazao mbalimbali kama kahawa, tumbaku, korosho na mazao mengine makubwa…lengo ni kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo bora kupitia uwezeshwaji kutoka NBC,” amesema.

Pia benki hiyo inatoa bima ya kilimo ili kufidia hasara kwa wakulima inayoweza kuwakumba kutokana na changamoto zisizotarajiwa za hali mbaya ya hewa, mafuriko na wadudu waharibifu wa mazao.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV