Uchaguzi Mkuu Kenya wakumbwa na dosari

August 9, 2022 10:28 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi ya watu katika baadhi ya maeneo hawapigi kura.
  • Sababu kubwa ni kukosewa kwa majina na picha za wagombea.
  • Uchaguzi wa ugavana wa Mombasa na Kakamega wasimama.

Dar es salaam. Wakati zoezi la kupiga kura likiendelea nchini Kenya leo, baadhi ya maeneo zoezi hilo limekumbwa na dosari, jambo lililosababisha upigaji kura kusimamishwa katika maeneo hayo ikiwemo Jimbo la Rongai.

Wapiga kura milioni 22 walijiandikisha kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu unaofanyika leo Agosti 9, 2022 nchini humo ambapo unawapa fursa ya kumchagua Rais na wabunge. 

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya, Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya ( IEBC) imesitisha uchaguzi wa wabunge na magavana katika maeneo manne nchi humo kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza ikiwemo karatasi za kura kutofautiana.

IEBC imesimamisha uchaguzi wa ugavana katika kaunti za Mombasa na Kakamega baada ya karatasi za kura kubainika kuwa na makosa kwa sababu maelezo na picha za wagombea hazikuwa sahihi.

Pia wapiga kura katika maeneo bunge mengine mawili ya Pokot Kusini na Kacheliba hawatampigia kura mbunge wao.


Soma zaidi:


Mchakato wa chapishaji wa karatasi za kupigia kura katika maeneo ambayo uchaguzi umesitishwa umeanza, na hivi karibuni tarehe za chaguzi katika maeneo hayo itatangazwa.

Hata hivyo, mchakato wa upigaji kura katika nyadhifa nyingine katika maeneo hayo unaendelea kama kawaida.

Upigaji kura kwa nyadhifa nyingine tano (Urais, Seneta, Mbunge, Mwakilishi wa Wanawake na Mbunge wa Kaunti) unaendelea kama ulivyopangwa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV