Uchaguzi Mkuu Kenya: Wachache wajitokeza kupiga kura

August 10, 2022 12:23 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni asilimia 56.17 ya waliojiandikisha ndiyo wamepiga kura jana.
  • Ni kiwango cha chini zaidi tangu uchaguzi wa vyama vyingi uanze mwaka tena 1992.

Dar es Salaam. Wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea nchini Kenya, imeelezwa kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ndiyo ambao wapiga kura wamejitokeza kwa kiwango kidogo tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa kuanzishwa tena nchini humo mwaka 1992.

Uchaguzi huo umefanyika jana Agosti 9, 2022 ambao Wakenya walipiga kura ya kumchagua Rais, Seneta, Mbunge, Mwakilishi wa Wanawake na Mbunge wa Kaunti

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), hadi zoezi la upigaji kura linahitimishwa jana jioni, wapiga kura milioni 12.06 kati ya milioni 22.1 waliojiandikisha walikuwa wamepiga kura. 

Hiyo ni sawa na asilimia 56.17 ya wapiga kura wote waliojiandikisha. Idadi hii haijumuishi waliotambuliwa kupitia rejista mwongozo (manual registration).

Hicho ni kiwango kidogo zaidi cha wapiga kura tangu mwaka 1992.

Uchaguzi ulioshuhudia idadi ndogo zaidi ya wapiga kura waliondikishwa ilikuwa mwaka 2002, ambapo asilimia 57 ya waliojiandikisha ndiyo walipiga kura. Hata hivyo, kiwango hicho kiko juu kidogo ikilinganishwa na mwaka huu. 

Uchaguzi ambao ulishuhudia kiwango cha juu cha wapiga kura tangu mwaka 1992 ilikuwa mwaka 2013 ambapo asilimia 86 ya wapiga kura waliojiandikisha ndiyo walipiga kura katika uchaguzi huo uliomweka madarakani Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto, ambaye ni mgombea katika uchaguzi wa mwaka huu akichuana vikali na Raila Odinga.


Soma zaidi

Ikumbukwe mwaka 2017, Rais Kenyatta alipokuwa akiomba kuchaguliwa tena, waliojitokeza kupiga kura walikuwa asilimia 78 ya waliojiandikisha huku katika uchaguzi wa mwaka 2007 ambao ulimweka madarakani Hayati Rais Mwai Kibaki ni asilimia 70 walijitokeza.

Uchaguzi huo wa 2007 uliitumbukiza Kenya katika machafuko makubwa ya kisiasa na kusababisha takribani watu 1,000 kulifariki dunia, baada pande zilizokuwa zikishiriki uchaguzi huo kutokukubali matokeo yaliyotangazwa.

Katika uchaguzi wa mwaka 1997 ni asilimia 68 ya wapiga kura ndiyo walijotokeza, huku uchaguzi wa mwaka 1992 ambao ulimuingiza marakani Rais Daniel Arap Moi ni asilimia 70 ya wapiga kura walioandikishwa walijitokeza kupiga kura.

Kumekuwa na sababu tofauti miongoni mwa wananchi hususani vijana, zilizosababisha mwitikio mdogo katika upigaji kuraikiwemo ukame uliopo kaskazini mwa nchi hiyo pamoja na Serikali kushindwa kutatua matatizo ya kiuchumi, kama kupanda kwa bei ya chakula na mafuta.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV