Si kweli: Tanzania haijazuia Kiswahili kufundishia shule za sekondari

January 14, 2023 10:28 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya baadhi ya watu kuzusha kuwa Kiswahili kisitumike sekondari.
  • Serikali yasema haijatoa tangazo hilo.

Dar es Salaam. Serikali imewataka wananchi kupuuzia taarifa zinazosambaa mtandaoni kuhusu kupiga marufuku lugha ya Kiswahili kufundishia shule za sekondari nchini na ukanda wa Afrika Mashariki.

Taarifa hiyo inayosambazwa na vyombo vya habari mbalimbali mtandaoni ikiwemo DW Africa na Nairobi News inasema Serikali ya Tanzania imepiga marufuku lugha hiyo kufundishia katika ngazi hiyo ya elimu ili kuwapa uwezo wanafunzi kujieleza vizuri kwa lugha ya Kiingereza jambo ambalo si kweli.

Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa, Serikali haijapiga marufuku matumizi ya lugha ya Kiswahili katika shule za sekondari na kwamba taarifa rasmi kuhusu uzushi huo zitatolewa hivi  karibuni.

Msigwa katika ukurasa wake wa Twitter ameongeza kuwa hivi sasa Tanzania inaendeleza juhudi zake katika kukuza na kuimarisha Kiswahili ndani na nje ya nchi hivyo marufuku hiyo ni sawa na kurudisha nyuma juhudi hizo.

“Tanzania inatambua wajibu wake wa kukuza matumizi ya Kiswahili duniani kote. Kwa hiyo, isingewezekana kwa Tanzania kupiga marufuku matumizi ya Kiswahili katika shule zetu zozote,” amesema Msigwa.

Nayo Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) inayoshughulikia na usimamizi na uendeshaji wa shule za msingi na sekondari nchini imeuwekea ujumbe huo maneno mekundu ’false information’ kwenye ukurasa wao wa Twitter ikimaanisha kuwa habari hiyo haina au ukweli.


Zinazohusiana


Tulichobaini

Taarifa hiyo inayosambaa mtandaoni imenukuu taarifa ya Benjamin Oganda anayetajwa kuwa Afisa Elimu Msaidizi katika ofisi ya Rais ambaye kiuhalisia hana mamlaka ya kubadili lugha ya kufundishia kwa ngazi yoyote ya elimu.

Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikithibitisha utekelezwaji wa lugha hiyo ya kujifunzia kwa shule za sekondari.

Kwa mujibu wa Sera ya elimu ya mwaka 2014 Lugha za Kiswahili, Kiingereza, lugha nyingine za kigeni na lugha ya alama zinatumika kufundishia masomo katika ngazi mbalimbali za elimu.

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV