Athari za muda mrefu za Uviko-19 kwa watoto

February 19, 2023 5:49 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Watu wengi wanaopata Uviko-10 watakuwa na dalili kwa muda mfupi ndipo watapona katika wiki chache. Muda wa kupona hotofautian kwa kila mtu. Inategemea jinsi ulivyoshambuliwa na ugonjwa huo na kama una ugonjwa mwingine mwilini. 

Baadhi ya watu wanapata matatizo ya afya ya muda mrefu baada ya kuugua na Uviko-19. Wakati mwingine ugonjwa huo husababisha mtu kujisikia mgonjwa kwa miezi mingi baada ya kuumwa mwanzoni. Hii inaitwa ‘Longcovid’. 

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), aina hii ya Uviko-19 inaweza kudumu kwa wiki nyingi na miezi mingi, hata baada ya mtu kutokuwa na virusi tena. Hata watu waliokuwa na maambukizi madogo ya Uviko-19 na kuhitaji kwenda hospitalini wanaweza bado kuwa na Uviko-19 wa muda mrefu.

Kwa watoto na vijana, dalili kama uchovu, hofu na kutoa harufu kali zinaweza kujitokeza. Muhimu ni kumpeleka mtoto hospitali ili akafanyiwe uchunguzi.

Enable Notifications OK No thanks