Dk Mpango: Siri ndiyo uhai wa Serikali

March 13, 2023 9:07 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Awaonya wakuu wa wilaya wanaovujisha siri kupitia mitandao ya kijamii.
  • Awataka kuwa walinzi wa siri kwa sababu ndiyo “uhai wa Serikali”.

Dar es Salaam. Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amesema wakuu wa wilaya wa Tanzania wana wajibu wa kulinda za siri za Serikali na kuhakikisha hazivuji kwa namna yoyote ile ikiwemo mitandao ya kijamii kwa sababu “ndiyo uhai wake”. 

Dk Mpango aliyekuwa akifungua mafunzo maalum kwa wakuu wa wilaya leo Machi 13, 2023 jijini Dodoma amesema moja ya majukumu ya viongozi hao ni kulinda siri za Serikali wakati wakitekeleza majukumu yao.

“Wakuu wa Wilaya itakupasa mzingatie kuwa siri ndiyo uhai wa Serikali, hivyo ni lazima kudhibiti uvujaji wa siri za Serikali,” amesema Makamu wa Rais. 

Kiongozi huyo amesema viongozi hao wanaweza kutunza siri za Serikali ikiwa wataepuka kabisa kutumia mitandao ya kijamii kama WhatsApp au barua pepe binafsi kutumiana  nyaraka za Serikali.

“Kuweni makini na maneno mnayozungumza, kupiga piga stori na wasaidizi wenu hususan madereva wetu na watu wengine mnapokuwa nje ya ofisini zenu au sehemu za starehe ili kuepuka kutoa siri za Serikali,” amesema Dk Mpango.


Zinazohusiana;


Licha ya kuwakumbusha kuhusu siri, Dk Mpango amewataka wakuu wa wilaya nchini kuacha kutumia wasaidizi na waandishi wa habari binafsi kwa sababu wanaweza kuhatarisha usalama wao wenyewe.

Baada ya kumaliza mafunzo hayo elekezi ya siku sita, Dk Mpango amewataka viongozi hao wakuteuliwa wakirudi katika maeneo yao wakadumishe nidhamu ya kazi, kutumia busara katika kusuluhisha migogoro lakini izingatie sheria na kanuni za nchi. 

Pia wameonywa kuacha kukaa ofisini bali wakutane na wananchi kujua na kutatua changamoto zao kwa wakati huku wakiweka kipaumbele katika usimamizi wa miradi ya maendeleo. 

“Msinyanyase walio chini yenu wana mazuri ya kusaidia kuboresha utendaji wenu wa kazi. Epukeni migogoro ya kiutendaji na viongozi wenzenu hasa wakurugenzi wa halmashauri. 

“Mhakikishe mnazingatia mipaka yenu ya madaraka na kazi na kwamba hatua mtakazochukua katika utendaji wenu vema zizingatie sheria, kanuni na taratibu za utendaji katika utumishi wa umma na Serikali,” amesisitiza Dk Mpango.  

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV