Bakita haijatoa ufafanuzi wa maneno haya

March 15, 2023 2:21 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni maneno yaliyojipatia umaarufu hivi karibuni.
  • Maneno ya ‘famasiala nini’, ‘famchezo nini’ pamoja na ‘fautani nini’.
  • Wazushi waghushi barua ya Bakita kukataza maneno hayo.

Dar es Salaam. Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita) limesema halijatoa ufafanuzi wowote kuhusu matumizi ya baadhi ya maneno yaliyojipatia umaarufu hivi karibuni ikiwemo ‘famasiala’.

Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter inayodaiwa kuwa ya Bakita inaeleza kuwa baraza hilo limepiga matumizi ya maneno ya ‘famasiala nini’ , ‘famchezo nini’ pamoja na ‘fautani nini’

Bakita kupitia ukurasa wao wa Twitter leo Machi 15, 2023 imesema taarifa hiyo siyo ya kweli.


Soma zaidi


Hii si mara ya kwanza kwa baadhi watu kughushi taarifa na mabango mbalimbali yanayotolewa na baraza hilo jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Huenda barua hiyo ya kughushi imetengenezwa kwa lengo la utani kutokana na maneno kama ‘famasiala nini’ , ‘famchezo nini’ pamoja na ‘fautani nini’ kujipatia umaarufu mkubwa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii licha ya kutokuwa sanifu.

Kwa mujibu wa Sheria namba 27 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza la Kiswahili pekee ndilo lenye mamlaka ya kutoa ufafanuzi wa matumizi sahihi ya maneno ya Kiswahili pamoja na kufanya usanifishaji wa meneno mapya.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV