Takukuru yanusa upigaji wa fedha za miradi Mwanza

May 29, 2023 2:00 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Yaagiza marekebisho kwenye miradi minne yenye gharama ya Sh3.3 bilioni
  • Ni miradi ya afya pamoja na elimu

Mwanza, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mwanza imebaini kasoro katika utekelezaji wa miradi minne yenye thamani ya Sh3.3 bilioni ambapo imetakiwa kufanyiwa marekebisho ili kuendana na thamani halisi.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, James Ruge aliyekuwa akizungumza na wanahabari Ofisini kwake  leo Mei 29, 2023 amewaambia kuwa wamebaini kasoro hizo baada ya kufuatilia miradi 42 ya maendeleo katika kada za afya, elimu, na maji yenye thamani ya Sh26 bilioni.

Miradi iliyobainika kuwa na mapungufu ni pamoja na mradi wa ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa Nje la zahanati ya Fumagila unaogharimu Sh131.5  milioni pamoja na mradi wa ujenz wa jengo la Wagonjwa wa ndani katika zahanati hiyohiyo wenye thamani ya Sh 122.2 milioni ambapo kulikuwa na ucheleweshaji wa malipo ma ununuzi wa vifaa.

“Tumemebaini usimamizi duni kwenye ujenzi wa shule ya Sekondari mpya ya Buhumbi wilayani Magu, unaogharimu Sh600 milioni ambao ulikamilishwa chini viwango na vifaa kuharibika,” amesema Ruge.

Mwanza inaendelea kukabiliwa na changamoto ya Rushwa katika utekelezaji wa miradi kwani ni miezi niwili tu imepita tangu Takukuru mkoani humo kubaini miradi 22 yenye thamani ya Sh6.5 bilioni kuwa na kasoro za utekelezaji.


Soma zaidi


Miradi hiyo ni sawa na asilimia 21 ya miradi 130 ya maendeleo katika sekta mbalimbali yenye zaidi ya Sh30.44 bilioni  inayotekelezwa mkoani humo.

Hali hiyo inaweza kusababisha wananchi kuchelewa kupata huduma muhimu za kijamii ikiwemo maji kuwawezesha kufanya shughuli za maendeleo na kuinua uchumi wa nchi.

Malalamiko 81 kuchunguzwa.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Takukuru amesema wanachunguza malalamiko 81 kati ya 90 ya vitendo vya  rushwa yaliyopokelewa katika kipindi cha Januari-Machi, 2023.

Katika kipindi hicho Jamhuri ilishinda kesi tatu kati ya nne na kesi mpya nne zilisajiliwa mahakamani na kufanya idadi ya kesi 18 zinazoendelea kusikilizwa.

Ruge amebainisha kuwa  katika kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu, wataendelea kuzuia vitendo vya rushwa kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufanya ukaguzi na kusimamia kwa karibu matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali.

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV