Takukuru yanusa upigaji miradi 22 ya maendeleo Mwanza

March 23, 2023 2:08 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Miradi 22 yenye thamani ya Sh6.5 bilioni imebainika kuwa na kasoro za utekelezaji.
  • Sekta zitakazoathirika na kasoro hizo za utekelezaji ni pamoja na elimu, afya, maji na ujenzi.
  • Takukuru yachunguza ili kuchukua hatua kwa wahusika. 

Mwanza. Miradi 22 yenye thamani ya Sh6.5 bilioni imebainika kuwa na kasoro za utekelezaji mkoani Mwanza, jambo linaloweza kuchangia kuchelewesha wananchi kujiletea maendeleo. 

Miradi hiyo ni sawa na asilimia 21 ya miradi 130 ya maendeleo katika sekta mbalimbali yenye zaidi ya Sh30.44 bilioni  inayotekelezwa mkoani humo.

Hali hiyo inaweza kusababisha wananchi kuchelewa kupata huduma muhimu za kijamii ikiwemo maji kuwawezesha kufanya shughuli za maendeleo na kuinua uchumi wa nchi. 

Kwa mujibu wa Ofisi ya Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, sekta zitakazoathirika na kasoro hizo za utekelezaji ni pamoja na elimu, afya, maji na ujenzi.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, James Ruge amesema taasisi hiyo imepokea taarifa 137 za miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoa Mwanza kati ya hizo, 80 zinalalamikiwa kugubikwa na vitendo vya rushwa.

“Taarifa za miradi hiyo tulizipokea kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka 2022 ambapo majadala 54 ya vitendo vya rushwa yamefunguliwa kati ya 80 yaliyokuwa yakichunguzwa kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa,” amesema Ruge.

Amesema kati ya majadala hayo 54 yanakamilishwa na 26 uchunguzi wa awali unaendelea.

“Serikali imetoa mabilioni ya fedha kwenye miradi ya maendeleo lengo ilete ustawi kwa wananchi kwa pamoja wananchi kwa ujumla wetu tunapaswa kufuatilia fedha za miradi hiyo kwa karibu ili lengo la Serikali litimie,” amesema Ruge.

Akizungumzia ujenzi wa vyumba 92 vya madarasa ya shule 12 za sekondari jijini Mwanza yanayojengwa kwa mfumo wa ghorofa kwa thamani ya Sh2.5 bilioni kasi yake ni ndogo hivyo Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza anapaswa kutoa fedha kulingana na makadilio huku pia kamati za ujenzi zizingatie sheria za manunuzi.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV