LHRC yabainisha mapungufu, suluhu mkataba wa bandari

June 14, 2023 5:32 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na masharti magumu ya usitishwaji wa mkataba na kutokuainishwa kwa  faida itakayopatikana wakati wa uwekezaji.
  • LHRC yaishauri Serikali kurejea vifungu vyenye mapungufu na kufanyia kazi.

Dar es Salaam. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeibua mapungufu ya mkataba wa ushirikiano kati ya Tanzania na Dubai katika uendelezaji wa bandari ikiwemo masharti magumu ya mkataba huku kikitoa mapendekezo ya namna ya kutatua mapungufu hayo.

Juni 10, 2023 Bunge la Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Anna Henga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC aliyekuwa akizungumza na wanahabari leo Juni 13, 2023 jijini Dar es Salaam amebainisha kuwa mkataba huo umeweka masharti magumu ya usitishwaji wake jambo ambalo linaweza kuibua migogoro ikiwa upande mmoja hautaridhishwa na utekelezaji wake.

“Ibara ya 23 kifungu cha pili inaweka sharti la kuendelea kwa mkataba hata baada ya kusitishwa kwa mkataba huu…ni wazi kuwa mkataba umeweka masharti magumu ya usitishwaji wake…

Ibara ya 22 kifungu cha nne inaweka katazo la nchi moja kujitoa katika mkataba huo katika mazingira yoyote…kifungu hiki kinamaanisha mkataba huu ni wa kudumu maisha yote na hakuna namna ya kujitoa au kuvunja,” amesema Henga.

Henga amebainisha kuwa upungufu mwingine katika mkataba huo ni kutokuainishwa kwa faida ambazo Serikali ya Tanzania inaweza kuipata katika kipindi chote cha uwekezaji.

Upungufu huo unaongeza hofu ya kuingia mkataba huu kwa kuwa hakuna mahali ndani ya mkataba unapoonesha matarajio ya faida itakayopatikana kila mwaka pia thamani ya jumla ya utekelezaji wa mkataba huo.

“Ni maoni yetu kuwa, kwa kuwa mkataba huu unaweka msingi kwa mikataba yote ya utekelezaji basi mikataba ya uwekezaji nayo iwekwe wazi ili umma uweze kujua thamani ya uwekezaji katika mradi huu,” ameongeza Henga.

Mapungufu mengine ya kimkataba yaliyobaishwa na LHRC ni pamoja na ibara ya 9 na 18 kutokuainisha kiwango cha juu na cha chini cha motisha na kikodi, masharti ya muwekezaji kutoingiliwa na kutobainisha aina ya uwekezaji na umiliki wa uwekezaji huo. 

Hata hivyo, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbarawa aliwaambia wabunge kuwa endapo watalipitisha azimio hilo miongoni mwa faida zitakazo patikana ni pamoja na kupungua kwa muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24 hali ambayo itavutia meli nyingi kwa kuwa gharama za kusubiri meli kupakuliwa mizigo zitapungua.

Kwa mujibu wa Mbarawa faida nyingine ni kuongezeka kwa idadi ya meli kutoka 569 mwaka 2021/22 hadi 2950 2022/23 pamoja na kuongezeka kwa ajira.


Soma zaidi


Suluhu za kuboresha mkataba

Pamoja na kuwepo kwa mapungufu ya kimkataba ambapo kwa mujibu wa LHRC yanaminya maslahi ya Serikali ya Tanzania kituo hiki kimetoa mapendekezo yatakayokuwa mzizi wa kuboresha mkataba huo ikiwemo kurekebisha mazingira ya kikodi.

“Mazingira ya kikodi ni muhimu yaainishwe bayana ili kuepeka mchakato wowote utakaoweza kutumia mwanya huo kwa maslahi binafsi na kuumiza maslahi ya umma,” amesema Henga.

Sambamba na pendekezo hilo LHRC imeitaka Serikali kurejea upya vipengele vya mkataba vyenye changamoto ya kisheria, hususan vile vilivyoibua mjadala mkubwa kwa wananchi. 

Aidha, LHRC imependekeza kuwekwa wazi kiwango cha umiliki wa sehemu ya uwekezaji huo ili wananchi kufahamu faida itakayopatikana katika uwekezaji huo husasani katika mikataba ya utekelezaji wa mradi.

Serikali kuendelea kupokea maoni

Spika wa Bunge la Tanzania Tulia Ackson aliyekuwa akizungumza mara baada ya wabunge kupitisha azimio hilo alisema kuwa licha ya kuwa azimio hilo limepitishwa bado wanaendelea kupokea maoni yatakayosaidia kuboresha utekelezaji wa mikataba itakayosainiwa.

“Wabunge wataendelea kuchangia na wananchi wataendelea kutoa maoni, mawazo waliyotoa wabunge ndio yanatakiwa kuweka msingi wa ile mikataba mingine inayokuja huko baadae, ili kuweka ule uwazi ambao unahitajika,” alisema Tulia.

Azimio la ushirikiano katika uendelezaji wa bandari kati ya Tanzania na Dubai limepokelewa kwa maoni tofauti na wadau ambao wamekuwa wakitoa maoni kuhusiana na mapungufu waliyoyabaini.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV