Mambo ya kuzingatia unapoanza ‘freelancing’ 2

September 2, 2023 11:32 am · Joshua
Share
Tweet
Copy Link
  • Sanaa ya mauzo na uhasibu ni nguzo muhimu.
  • Kuajiriwa ni msingi mzuri wa nidhamu ya kujiajiri.
  • Pia nidhamu, uaminifu na kuwajua wateja wako vizuri.

Dar es Salaam. Uwezo wa kufanya kazi kokote ulipo duniani unamhitaji freelancer (mfanyakazi wa kujitegemea) kuwa na msingi mzuri wa usimamizi wa biashara ya huduma ili iweze kufanikiwa. Msingi huu unajengwa katika usimamizi mzuri wa fedha, mawasiliano na nidhamu binafsi.

Katika makala iliyopita tuliangazia kwa nini uwe ‘freelancer’ na changamoto zinazoambatana na ajira huru. Wiki hii tunaendelea  kuangazia mambo ya msingi ya kuzingatia unapoanza ‘freelancing’. Twende pamoja!

Fuata sheria na kanuni za nchi

Sheria na taratibu za kufanya biashara Tanzania zinamlazimu mfanyabishara kujisajili na mamlaka tofauti ikiwemo Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ili kusajili jina la biashara na Mamlaka ya Mapato (TRA) ili kupata namba ya mlipa kodi (TIN).  

Freelancer maarufu nchini Tanzania, Baraka Mafole ameiambia Nukta Habari (www.nukta.co.tz) kuwa kufuata taratibu za kisheria (compliance) ni kipimo cha biashara iliyoimarika. Freelancing ni biashara kama biashara zingine, kwa hiyo ni muhimu izingatie sheria na kanuni za nchi hasa zinazohusu kodi. 

Mathalan, kila mtoa huduma anapaswa kuwa na Namba ya Mlipa Kodi (TIN ili kumuwezesha kulipa kodi kwa mapato anayoingiza ikiwemo yale ya kazi ya freelancing. 

“Baada ya muda nilianza kukua katika biashara, nikawa nakutana na taasisi zilizokua zikinunua huduma yangu. Walinitaka niwe na risiti za kodi. Ilinibidi nisajili Namba ya Mlipa Kodi (TIN) pamoja na kununua mashine ya kutolea risiti (EFD) ambayo inasaidia kwenye ukaguzi wa hesabu za mapato na matumizi,” anasema Mafole. 

Ujuzi wa lugha 

Kujua lugha ya Kiingereza kunakupa nafasi ya kuwasiliana na wateja hasa wa kimataifa kwa njia rahisi. Karibu huduma zote za uuzaji wa bidhaa mtandaoni hufanyika kwa Kiingereza, hivyo freelancers wana wajibu kuifahamu lugha hii vizuri ili kuwapata wateja kwa urahisi.

“Kazi zinazohusisha mawasiliano kama vile kutafsiri, mauzo na masoko mitandaoni, Kiingereza ni kipaumbele cha lazima tofauti na kazi za kiufundi kama utengenezaji wa filamu, kupiga picha, au udereva.” anaongeza Baraka ambaye amekua freelancer tangu mwaka 2020.


Soma zaidi


Tafuta mhasibu 

Albany James mwanzilishi wa Foodsasa, tovuti ya kuagiza chakula mtandaoni, inayounganisha watu na migahawa anasema changamoto kubwa kwa freelancers ni nidhamu kwa kuwa hawasimamiwi na mtu. 

Anasema baadhi yao huwa na matumizi makubwa kuliko mapato yao, jambo linalochangia wasipige hatua na kukuza biashara zao katika viwango vya kimataifa na kushindwa kutoa huduma bora kwa wateja wao kwa sababu ya ukosefu wa mitaji.

Kuingia na kupotea kwa pesa katika ‘freelancing’ ni jambo linalotokea usipokuwa makini kutunza rekodi za mapato na matumizi. Picha|Freepik

“Nilikua nasumbuka kukusanya pesa kutoka kwa wateja kati ya 15 hadi 18 kwa wakati mmoja.  Ndipo nilipotafuta mhasibu wangu binafsi amabae ninamlipa na imenisaidia kuzingatia mambo mengine ikiwemo bidhaa na vibarua,” anasema James na kuongeza kuwa nishamu ya pesa ni ujuzi muhimu anaotakiwa kuwa nao freelancer. 

James anashauri vijana wanaotaka kujiajiri mtandaoni kuwa ni vema wapate ajira ya kuajiriwa kwanza kisha waingie katika tasnia ya freelancing wakiwa wamejiandaa kifikra.  

Ifahamu sanaa ya kuuza

Mshindi wa tuzo za utengenezaji filamu  Nick Kyriakides, ameeleza katika ukurasa wake wa Linkedin kuwa “kuuza ni kuweza kumshawishi mteja kuwa na mtazamo sawa na wako ili anunue huduma na bidhaa yako. Adhma kuu ya mauzo ni kufaidika kwa pande zote mbili.

“Freelancers wengi wameweka fikra katika kuuza ili kuingiza mapato lakini ni muhimu kufikiria na kufahamu nini utapata katika mchakato huo.”

Kyriakides anasema wateja hununua suluhu ya matatizo au changamoto zao. Hivyo ni muhimu kwa freelancers kujikita katika kutoa huduma ya ujuzi au maarifa au bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na zinazokidhi mahitaji ya kila mteja mtandaoni.  

Hata hivyo, anasisitiza kuwa yote hayo hayatawezekana ikiwa hakutakuwa na nidhamu, uaminifu wa biashara. 

Je wewe freelancer au una ujuzi wowote ungependa kushare nasi? Unaweza kuwasiliana na sisi kupitia kupitia barua pepe newsroom@nukta.co.tz au kwa nambari ya simu 0677 088 088.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV