Apps zitakazokusaidia kuboresha akaunti yako ya Instagram

November 15, 2021 1:57 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na Canva, Pixelcut na Instories.
  • Zinatengeneza picha kulingana na vipimo vinavyohitajika na mtandao huo.
  • Mpangilio mzuri wa ukurasa  wako itakuongezea umakini kwa wateja wako.

Dar es Salaam. Kwa mfanyabiashra wa mtandaoni, muonekano wa ukurasa wako wa Instagram ni muhimu. 

Mimi kama mteja wako, muonekano wa ukurasa wako utanipatia fikra ya kuwa umejipanga vema na siyo mbabaishaji wala kanjanja kama wengine.

Inaanza na jinsi picha na video zako zinavyoonekana na mpangilio wa maudhui hayo kwenye mtandao huo wa kijamii.

Ili kuhakikisha ukurasa wako wa biashara kwenye mtandao wa Instagram unavutia, zipo programu tumishi (app) ambazo zinaweza kukusaidia kuboresha ukurasa wako kwa gharama ndogo au bure kabisa.

App hizi zinaweza kutumika kwenye simu na kuondoa ulazima wa kuajiri mtaalamu wa grafiki kukusaidia kutengeneza matangazo kwa ajili ya mitandao ya kijamii kama Instagram. 

Unaweza kuchagua muundo unaokufaa na kuutumia kwenye ukurasa wako. Picha| Canva.

Canva

App hii inatumika kutengeneza picha kwa takriban mitandao yote ya kijamii ikiwemo Instagram, Twitter na Linkedin.

Canva inazingatia vipimo husika vya picha unayotaka kupakia kwenye mtandao wa kijamii ikiwemo picha za juu ya wasifu wako yaani headers kwa mitandao kama Facebook, Twitter na Linkedin.

Kwa picha za kawaida, Canva inazitengeneza kwa uwiano wa kuonekana vizuri hata kabla mtu hajaibonyeza kuiona kwa ukubwa.

App ya Canva inaambatana na mifano (layouts) ya picha ambazo unaweza kuzitengenezea picha zako.

PixelCut

Kuna wakati ambapo unataka umakini uwe kwenye bidhaa yako tu na siyo kitu kingine. Unaweza elewa nini nazungumzia kama ulishawahi kupost picha ya miwani ipo karibu na kikombe na mtu akaulizia kikombe.

App ya Pixelcut inasaidia kuondoa vitu vyote ambavyo hauvihitaji kwenye picha yaani background. 

Kupitia app hii, unaweza kubadilisha rangi iliyo nyuma ya bidhaa unayotaka kupost na pia kuandika maneno unayoyahitaji katika bidhaa hiyo kama punguzo la bei.

Ukitumia app hii huenda ukaepuka kuweka handle yako ya instagram katikati ya video na kuiweka kwa unadhifu kama mfanyabiashara mwenye weledi.

App zingine ni pamoja na Loopsie, unfold, Over na Life Lapse. Picha| Buzzing Blonde.

Instories

Umewahi kujaribu kuweka muziki kwenye video yako na mambo yakagoma? Ukajaribu kuwasha redio yako kuunga unga ili video yako iwe na sauti na matokeo yakawa siyo ya kufurahisha?

App ya Instories inakusaidia kama mfanyabiashara kutengeneza video na picha za bidhaa zako zikiwa na muonekano mzuri na kwa kipimo kinachotakiwa mfano vipimo vya video fupi za reels, video za stories na hata post za kawaida.

Uzuri ni kuwa, kuna mifumo (layouts) ya bure na zingine ambazo utahitaji kulipia.

App hii pia inaambatana na nyimbo mbalimbali za sekunde 30 lakini unaweza kupakia muziki wako unaoupenda.

Programu hizi zinapatikana kwenye maduka ya apps na zote zina mfumo wa bure na mfumo ambao unaweza kulipia.

Teknolojia imekuja na mambo mengi na kama mfanyabiashara, usikubali kuachwa nyuma.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV