Rais Samia ateua Naibu Kamishna Mkuu TRA
- Amemteua Mcha Hassan Mcha kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mcha Hassan Mcha kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Jaffar Haniu katika taarifa yake iliyotolewa leo Januari 18, 2022 amesema kuwa Mcha anachukua nafasi ya Msafiri Lameck Mbibo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Madini.
Kabla ya uteuzi huo Mcha alikuwa Kamishna wa Udhibiti na Utekelezaji (Control and Enforcement) Makao Makuu ya TRA.
Pia, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Samia amemteua Balozi Celestine Joseph Mushy kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria.
Balozi Muhy alikuwa Katibu Tawala Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Latest