WhatsApp kuwaongezea nguvu ya udhibiti “maadmin”

August 3, 2022 12:29 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Inatarajia kuanzisha kipengele kipya cha wao kufuta ujumbe wa kila mtu kwenye kundi.
  • Itasaidia kuweka nidhamu kwenye makundi na kupunguza maudhui yasiyohusika.   

Dar es Salaaam. Mtandao wa kijamii wa WhatsApp siku zijazo utawaongezea nguvu viongozi wa makundi ya mtandao huo kuwa na uwezo wa udhibiti ikiwemo kufuta ujumbe wa watumiaji wa makundi hayo.

Kwa mujibu wa tovuti ya WABetaInfo, mtandaoni huo unafanyia majaribio kipengele kipya kinachojulikana kama “admin detele” kwa baadhi ya watumiaji wa simu zenye mfumo endeshi wa Android.

Kipengele kipya cha Admin delete kitawaruhusu wasimamizi wa kikundi kufuta ujumbe wowote wa washiriki katika kikundi chao.

Hiyo huend aikasaidia kuongeza nidhamu katika makundi hayo na kuzuia maudhui yasienda na malengo ya kuanzishwa kwa kundi husika. Hata hivyo, kipengele hicho kisipotumika vizuri kinaweza kuvunja haki za watumiaji wa mtandao huo ikiwemo uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.


Soma zaidi:


Admin akifuta ujumbe wa kikundi utatoweka kwa kila mtu, na kuacha taarifa kwamba umefutwa na msimamizi.

Kipengele kingine kipya kizuri kinachofanyiwa kazi ni Chatbot, ambacho kitawanufaisha watumiaji wa matangazo ndani ya programu hiyo. 

Matangazo hayo yatajumuisha arifa (notification) kuhusu vipengele vipya vya WhatsApp, vidokezo na mbinu, na ikiwezekana ujumbe kuhusu ofa zinazolipishwa. 

Kumbuka pia mapema mwaka huu, WhatsApp ilianza kujaribu kipengele kingine ili kuboresha matumizi ya mtumiaji, kuwezesha uwezo wa kuhariri ujumbe wako.

/
No matches found for this filter
30 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV