China haitafungua kituo cha polisi Tanzania

October 20, 2022 9:39 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Balozi abainisha hakuna mkataba wa ushirikiano wa kipolisi kati ya China na Tanzania. 
  • Afafanua ni lazima kuwe na makubaliano maalumu yenye malengo mahususi.

Dar es salaam. Watanzania wametakiwa kupuuzia taarifa iliyotolewa na idhaa ya kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa  nchi ya China ina mpango wa kufungua kituo cha polisi barani Afrika ikiwemo Tanzania.

Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amekanusha madai hayo kwa kueleza kuwa taarifa hiyo iliyonukuliwa kutoka baadhi ya vyombo vya habari nchini Nigeria siyo ya kweli bali ina lengo la kuleta sintofahamu.

“Niwahakikishie hizi ni habari za uongo. Sisi kama Tanzania hatuna mkataba wowote wa mahusiano ya ushirikiano wa kipolisi ambao unapelekea kufungua vituo vya polisi kama ilivyodaiwa, hatujaomba wala wao hawajatuomba,” amesema Kairuki.

Balozi  Kairuki amesisitiza kuwa ni kweli upo utaratibu wa nchi moja kufungua kituo cha polisi kwenye taifa lingile lakini lazima kuwe na makubaliano maalum baina ya mataifa hayo kwa madhumuni mahususi.

“China ina makubaliano na nchi ya Italia ya polisi wake kufanya kazi katika nchi hiyo na dhumuni lake lilikuwa kukidhi mahitaji ya maelfu ya watalii wa China waliokuwa wanaenda kutalii katika jiji la Milan,” amesema.

Aidha Kairuki amesikitishwa na kitendo cha BBC kutumia vyanzo visivyo vya kuaminika kuandika habari zake jambo ambalo linashusha heshima ya shirika hilo kongwe duniani.

Taarifa  iliyochapishwa katika tovuti ya BBC na ukurasa wa mtandao wa Twitter  siku ya jumanne Oktoba 18 mwaka huu ilieleza China imekuja na mpango huo ili kudhibiti vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na raia wake katika nchi za Tanzania, Nigeria na Lesotho.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV