Majaliwa: Njooni muwekeze Tanzania

October 26, 2022 12:24 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Awaomba wawekezaji wa Korea Kusini kujenga viwanda vya dawa nchini. 

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kutokana na mpango wa Serikali wa kuendelea kuimarisha eneo la utoaji huduma za afya, Tanzania inawakaribisha wawekezaji kutoka Korea Kusini kwa ajili ya kujenga viwanda vya dawa na vifaa tiba ili kuwezesha upatikanaji rahisi wa dawa na vifaa tiba. 

               

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Oktoba 26, 2022 baada ya kushuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) na Serikali ya Jimbo la Chungcheongbuck nchini Korea kusini.

Sehemu ya makubaliano katika mkataba huo ni kujadili na kuendeleza mahusiano ya kibiashara katika nyanja za masoko ya bidhaa zinazozalishwa na Makampuni ya dawa katika jimbo hilo.

Maeneo mengine ni kubadilishana watumishi, semina za pamoja za wataalamu wao katika nyanja mbalimbali, kubadilishana na kupeana taarifa za uwekezaji kwenye sekta ya dawa, msaada wa kitaalamu na wataalam.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Nyumba nafuu Dar zinavyowasukuma wakazi kwenye maeneo hatarishi

Nyumba nafuu Dar zinavyowasukuma wakazi kwenye maeneo hatarishi

Nukta TV

Haya ndio maajabu ya iPhone Duo simu mpya kutoka Apple

Haya ndio maajabu ya iPhone Duo simu mpya kutoka Apple

Nukta TV

Kitakachotokea IGP, CDF na DCI wasipofika mahakamani kesi ya Lissu

Kitakachotokea IGP, CDF na DCI wasipofika mahakamani kesi ya Lissu

Nukta TV