Ndege ya Precision Air yaanguka ziwani, Rais Samia akiwaomba Watanzania utulivu

November 6, 2022 8:46 am · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link
  • Rais Samia Suluhu Hassan awasihi Watanzania kuwa na utulivu wakati vikozi vya ukoaji vikiendelea kuwaokoa waliohusika katika ajali hiyo.

Dar es Salaam. Ndege ya Shirika la Ndege la Precision Air imeanguka kwenye Ziwa Victoria baada ya kukumbukwa na hali mbaya ya hewa wakati wa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba huku Rais Samia Suluhu Hassan akiwataka Watanzania kuwa watulivu wakati uokoaji ukiendelea.

Taarifa za kuanguka kwa ndege hiyo katika ziwa hilo kubwa zaidi barani Afrika zilianza kusambaa mtandaoni mapema asubuhi ya Jumapili, Novemba 6, 2022 majira ya Saa 3 kabla ya mamlaka kuthibitisha ajali hiyo.

Precision Air imesema ndege hiyo namba PW 494 iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam ilipata ajali wakati ikianza kutua katika uwanja huo uliopo kandokando mwa Ziwa Victoria.

“Kikosi cha waokoaji kimepelekwa eneo la ajali na taarifa zaidi tutazitoa baada ya muda wa saa mbili,” kampuni hiyo ya ndege imeeleza katika taarifa yake kwa umma.

Rais Samia amesema amepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo na kuwatumia salamu za pole watu wote walioathirika na ajali hiyo.

“Tuendelee kuwa watulivu wakati huu zoezi la uokoaji likiendelea huku tukimuomba Mwenyezi Mungu atusaidie,” amesema Rais Samia.

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limeeleza kuwa ndege hiyo ilianguka ziwani baada ya kuathiriwa na upepo mkali na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa huo wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

TBC imesema kuwa mashuhuda wameeleza kuwa watu zaidi ya 15 wameokolewa na kukimbizwa moja kwa moja katika Hospitali ya Kagera huku vikosi vya uokoaji vikiendelea kuwaokoa wengine waliosalia ndani ya ndege inayoelea ziwani. Hadi sasa idadi ya waliohusika katika ajali hiyo haijawa bayana.

Video zilizochapishwa na TBC zinaonyesha kuwa vikosi vya uokoaji vinaendelea kuokoa huku boti ndogo zikivuta ndege hiyo kuelekea eneo la ufukwe wa Ziwa Victoria.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV