Senegal yaufungia mtandao wa TikTok kwa madai ya kuchochea ghasia

August 4, 2023 8:13 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema matumizi yake yanatishia usalama wa nchi
  • Yaungana na mataifa ya Ulaya pamoja na America ambayo mtandao huo umepigwa marufuku.

Dar es Salaam. Senegal imezuia matumizi ya programu ya mtandao wa kijamii wa TikTok kutokana na madai ya kueneza jumbe za chuki na uasi baada ya kufungiwa kwa chama kikuu cha upinzani na kumweka kizuizini kiongozi wake Ousmane Sonko.

Senegal imekua nchi ya kwanza barani Afrika kuzuia matumizi ya mtandao huo wa kijamii, ambapo zuio hilo linakuja baada ya kufungwa pia kwa huduma za intaneti siku ya  jumatatu Julai 31, 2023.

Waziri wa Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali wa Senegal, Moussa Bocar Thiam amebainisha kuwa wameufungia mtandao huo maarufu duniani baada ya kubaini kuwa matumizi yake yanatishia usalama wa nchi.

“Imebainika kuwa programu TikTok ni mtandao wa kijamii unaopendelewa na watu wenye nia mbaya kusambaza jumbe za chuki na uharibifu zinazotishia utulivu wa nchi,” amesema Thiam.

Senegal inaungana na baadhi ya taasisi na mataifa ya Ulaya Na Marekani  ambayo yameupiga marufku mtandao huo ikiwemo tume ya Umoja wa Ulaya (EU),  Marekani yenyewe pamoja na Canada.


Soma zaidi


Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017, TikTok umegeuka kuwa mtandao pendwa hususan na vijana ambao wamekuwa wakibuni maudhui mbalimbali kwa njia ya video ambapo hutumia kama njia mojawapo ya kujipatia kipato na burudani.

Kupitia mtandao huo watu kadhaa wamejizolea umaarufu nchini Tanzania kutokana na aina ya maudhui wanayochapisha akiwemo Mtanzania Killy Paul ambaye alipata fursa ya kwenda kutumbuiza kwenye tamasha la muziki nchini India kupitia mtandao huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), mtandao wa Tiktok mwaka 2021 ulipiku watumiaji mtandao wa Google jambo ambalo halikuwahi kufanyika kwa miaka 10 iliyiopita.

Mpaka sasa mtandao huo umepakuliwa na watu zaidi ya bilioni 1 duniani kote na kuufanya kuwa mtandao uliopakuliwa zaidi ukifuatiwa na mtandao wa Instagram na Facebook.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Takwimu ya robo ya pili ya mwaka (Aprili-Juni)ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Tiktok ilishika nafasi ya tatu katika orodha ya mitandao iliyotumiwa zaidi nchini ikiwa na jumla ya gigabaiti milioni 33.3.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV