21 Bridges yamgeuza Blackpanther kuwa askari mpelelezi

December 6, 2019 8:55 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Je, majambazi hao (Stephan James na Taylor Kitsch) watapatikana pale Madaraja 21 ya Manhattan yatakapofungwa, au mito mitatu ya jiji hilo itakapo wekwa chini ya ulinzi?. Picha| Youtube.

  • Ni filamu mpya kwenye kumbi za sinema
  • Inasimulia kisa cha mtoto aliyejifua kuwa askari mpelelezi baada ya baba yake kuuwawa na majambazi.
  • Filamu imegharimu zaidi ya Sh75.8 bilioni kukamilika.

Dar es Salaam. Baada ya kunyonga tai wiki nzima, kujaza akili yako na mambo ya kikazi, unastahili kujipatia mapumziko yatakayokufanya ushushe pumzi. 

Ni aje ukipalia pensi na raba yako na ukatoka na familia yako kutazama filamu kwenye kumbi za sinema wikiendi hii? Haya ndiyo mapendekezo ya filamu gani inafaa.

21 Bridges

Baada ya kumfahamu kama Black Panther, sasa Chadwick Boseman amerudi kama askari mpelelezi. 

Pale maaskari nane wanapouawa na majambazi, Chadwick analazimika kuwatafuta majambazi hao na kama mbobezi wa fani hiyo anayeaminika na jiji zima la NewYork, anatakiwa awe amewatia nguvuni kabla masaa matano hayajatimia.

Je, majambazi hao (Stephan James na Taylor Kitsch) watapatikana pale Madaraja 21 ya Manhattan yatakapofungwa, au mito mitatu ya jiji hilo itakapo wekwa chini ya ulinzi?

Zaidi, jitihada zao zitafua dafu hata pale treni zote na Subway zote zitakapo fungwa?

Hakika unahitaji kujua nini kitatokea baada ya jiji zima kufurikwa na sare za polisi huku ving’ora vikilia kuashiria hali ya tahadhari kwenye filamu hii iliyoandaliwa chini ya bajeti ya Sh75.8 bilioni.

Bunduki na risasi zinazosababisha damu na miili kutapakaa kwenye ardhi ya Manhattan ni chumvi tosha kwenye filamu hii iliyoandaliwa na Brian Kirk ambaye pia ameongoza filamu ya “My boy Jack”. 


Zinazohusiana


Nunua tiketi yako kwas Sh10,000 tu kwenye sinema za Mlimani City na Aura Mall na zinginezo.

Hata hivyo, kama hii siyo upepo wako, bado Frozen na filamu zingine kedekede zinaendelea kuonyeshwa kwenye runinga ambayo Century Cinemax ya Mlimani City wanadai ni kubwa kulizo zote Afrika Mashariki.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Nukta TV

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV