Zuhura Yunus: Mkurugenzi mpya Mawasiliano Ikulu

February 1, 2022 7:50 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Anachukua nafasi ya Jaffar Haniu ambaye atapangiwa kazi nyingine.
  • Zuhura alikuwa mtangazaji wa BBC Swahili kabla ya uteuzi huo.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Zuhura Yunus Abdallah kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Kabla ya uteuzi huo, Zuhura alikuwa Mtayarishaji wa Vipindi na Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Rekodi aliyoiacha Zuhura ambaye alifanya kazi BBC kwa miaka 14 tangu mwaka 2008 ni kuwa mwanamke wa kwanza kutangaza kwenye kipindi cha Dira ya Dunia.

Uteuzi wake ya kuondoka BBC na kuandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Zuhura anachukua nafasi ya Jaffar Haniu ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Haniu anaachia nafasi hiyo baada ya kudumu kwa takriban miezi nane tangu ateuliwe Juni 2021 akichukua nafasi ya Gerson Msigwa ambaye sasa ni Msemaji Mkuu wa Serikali.

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu amesema uteuzi huo umeanza Januari 30, 2022.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV